EATV AWARDS FULL SHOW - 2016
Автор: EastAfricaTV
Загружено: 2017-01-03
Просмотров: 13985
Описание:
TUZO za EATV zimeanzishwa mwaka 2016 na kampuni ya East Africa Television na Radio, zimefanyika kwa mara ya kwanza tarehe 10/12/2016 jijini Dar Es Salaam,Tanzania.
Tuzo hizi mwaka 2016 zimeshirikisha wasanii wa muziki na filamu kutoka nchi za Afrika Mashariki na zitakuwa zikifanyika kila mwaka, huku vipengele vya tuzo vikiongezeka kila mwaka kutoka vipengele kumi vilivyoshindaniwa mwaka huu. Kuanzishwa kwa tuzo hizi kuna lengo la kuthamini wasanii na kuleta ushindani kwenye sekta hii ya sanaa kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki. Kwenye za mwaka 2016 kulikuwepo na jumla ya vipengele kumi. Vipengele sita vilishindaniwa na wasanii wa muziki, Vipengele vitatu vilishindaniwa na wasanii wa filamu na kipengele kimoja ilikua ni tuzo ya heshima. Vipengele hivyo kwa upande wa muziki ni mwanamuziki bora wa kiume, mwanamuziki bora wa kike, mwanamuziki bora Chipukizi, kundi bora la mwaka, Video bora ya mwaka na Wimbo bora wa mwaka.
Kwa upande wa Filamu vipengele vilivyoshindaniwa ni Filamu bora ya Mwaka, Muigizaji Bora wa Kiume na Muigizaji Bora wa kike.
Tuzo za EATV 2016 zimefanyika kwa udhamini wa Coca Cola, Barclays Bank Tanzania na Vodacom Tanzania .
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: