BALAA LA MAKONDA ARUSHA: LEO NI KUCHINJA NA KULA NYAMA BURE
Автор: Gilly Bonny Tv
Загружено: 2024-11-28
Просмотров: 8774
Описание:
Kufuatia uwepo wa ugeni mkubwa wa Marais wa nchi nane Jijini Arusha, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Makonda, ameandaa hafla maalum itakayohusisha kuchinja, kula nyama, kupata vinywaji, na burudani mbalimbali.
Hafla hiyo inafanyika leo tarehe 28 Novemba 2024 katika eneo la karibu na Ofisi za Mkuu wa Mkoa, ambapo wananchi na wageni watapata fursa ya kufanya biashara.
Mkoa wa Arusha umejaa ugeni mkubwa, ikiwa ni pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye atakuwa mwenyeji wa Marais wengine saba wa nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Maadhimisho haya ni ya kipekee kwani yanasherehekea miaka 25 tangu kuundwa kwa Jumuiya hiyo ya Kikanda, lengo likiwa ni kuimarisha ushirikiano na mshikamano miongoni mwa nchi wanachama.
Wananchi wa Arusha na baadhi ya wanufaika wa ugeni huu, akiwemo wanyama chanya, wamesema kuwa wanashukuru kwa fursa hiyo ya kipekee na wameonyesha furaha yao kutokana na umuhimu wa tukio hili.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: