MAANDAMANO TUNDUMA,WAFANYABIASHARA WAPINGA ALIYEONDOLEWA NA MKUU WA WILAYA KURUDI SOKONI.
Автор: SONGWE TV1
Загружено: 2024-04-11
Просмотров: 517
Описание:
KARIBU KUTAZAMA VIPINDI VYETU KATIKA MITANDAO YA KIJAMII SONGWE TV1
KWA MAWASILIANO PIGA SIMU NO 0622 010846 Karibu SONGWE TV1 kwa habari na matukio kiganjani mwako WAFANYABIASHARA WAANDAMANA KUPINGA ALIYEONDOLEWA NA MKUU WA WILAYA KURUDI SOKONI.
Wafanyabiashara wadogo katika Soko la majengo Halmshauri ya mji Tunduma mkoani Songwe wameandamana,baada ya Mfanyabiashara Mwenzao aliyeondolewa kwa tuhuma mabalimbali kurudi Sokoni hapo.
Inadaiwa kuwa Swaumu Njeje mfanyabiashara wa Samaki aliondolewa Sokoni kwa Amri ya mkuu wa wilya ya Momba baada ya kuonekana anasababisha migogoro na kuzua taharuki sokoni.
Inadaiwa kuwa Mkuu wa wilaya alichukua maamuzi hayo tarehe 28 January na kumuamuru Swaumu kuondoka Sokoni kwa kulinda Usalama wake pamoja na Wafanyabiashara wengine Baada ya kuwashitaki mahakamani wafanyabiashara zaidi ya 20 kwa kuwatuhumu kutishia Kumuua na Swaumu alitii Amri ya Mkuu wa Wilaya.
Wafanyabiashara hao wameandamana kwenda ofisi za Soko kuwataka viongozi kumuondoa Mara moja Swaumu baada ya kurudi sokoni bila ridhaa ya wafanyabiashara wa Soko
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: