ycliper

Популярное

Музыка Кино и Анимация Автомобили Животные Спорт Путешествия Игры Юмор

Интересные видео

2025 Сериалы Трейлеры Новости Как сделать Видеоуроки Diy своими руками

Топ запросов

смотреть а4 schoolboy runaway турецкий сериал смотреть мультфильмы эдисон
Скачать

MADEREVA WA MALORI WALIA KUVAMIWA DRC, CODECO WATAJWA

Автор: Mwananchi Digital

Загружено: 2025-02-24

Просмотров: 5814

Описание: Madereva wa malori kutoka nchi nne wamedai kuvamiwa na watu waliovalia sare za kijeshi walipokuwa wakisubiri kuvuka mpaka kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Zambia, katika eneo la Kasumbalesa, Lubumbashi.

Uvamizi huo umetokea usiku wa kuamkia jana Jumapili, Februari 23, 2025 takriban kilometa 10 kabla ya kufika mpakani, huku malori yakiwa yamesimama kwenye foleni ya kuvuka mpaka.

Akizungumza na Mwananchi kupitia ujumbe mfupi wa simu, Balozi wa Tanzania nchini DRC, Said Mshana, amesema bado hajapokea taarifa rasmi kutoka kwa madereva au viongozi wao lakini anaendelea kufuatilia suala hilo.

"Nafuatilia, sijapata taarifa yoyote kutoka kwa viongozi wao wala dereva yeyote," amesema Balozi Mshana.

Juma Mohamed, mmoja wa madereva waliokuwepo eneo la tukio, ameiambia Mwananchi kuwa wavamizi hao waliwataka madereva wawape fedha na chakula.

“Hapa jirani kuna mlima ambao unasemekana kuwa kambi ya jeshi. Walikuja wakiwa wamevalia sare za kijeshi, wakatoa amri ya kupewa chakula, pesa na simu. Dereva aliyekataa alishambuliwa na vioo vya magari vilivunjwa. Walioathirika zaidi ni madereva kutoka Tanzania na Zambia,” amesema Juma.

Kwa sababu ya foleni ndefu katika mpaka huo, madereva wamelazimika kuegesha magari yao hadi maeneo ya porini, kwa sababu mpaka huo hufungwa saa 12 jioni na kufunguliwa saa moja asubuhi kwa saa za DRC.

Juma amesema madereva waliovamiwa walikuwa wanasafirisha mizigo kutoka DRC baada ya kushusha mizigo yao ya awali. Malori yaliyoshambuliwa yalitokea Tanzania, Zambia, Zimbabwe na Afrika Kusini.

“Lakini ilipofika saa 5 asubuhi, magari yalianza kuruhusiwa kupita ingawa msongamano ulisababishwa na vurugu za usiku huo,” amesema dereva huyo.

Dereva mwingine, aliyejitambulisha kwa namba ya D1186, amesema kupitia mawasiliano na viongozi wa madereva, wavamizi walikuwa na silaha na walifyatua risasi kiholela.

“Tumepata uvamizi hapa. Madereva wote tulilazimika kukimbia. Walikuwa wakifyatua risasi ovyo na kupora mali zetu. Wakimkuta dereva kwenye gari, walimchukulia kila kitu,” amesema.

Kwa kuhofia usalama wao, amesema baadhi ya madereva walikimbilia msituni, “lakini waliporudi, walikuta vioo vya magari yao vimevunjwa. Wengi walikimbilia tena msituni kwa kuhofia wavamizi hao kurudi tena.”

Amesema kutokana na taharuki iliyokuwapo, baadhi ya magari yaligongana, kwa sababu madereva hawakuelewa hali halisi ya usalama na kama waliovamia walikuwa wanajeshi halisi au watu waliovaa sare zao.

Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Malori ya Kati na Madogo Tanzania (Tamstoa), Chuki Shabani amesema matukio ya uvamizi kwa madereva Congo si jambo geni.

Imeandaliwa na Mgongo Kaitira kwa msaada wa Mashirika.

Не удается загрузить Youtube-плеер. Проверьте блокировку Youtube в вашей сети.
Повторяем попытку...
MADEREVA WA MALORI WALIA KUVAMIWA DRC, CODECO WATAJWA

Поделиться в:

Доступные форматы для скачивания:

Скачать видео

  • Информация по загрузке:

Скачать аудио

Похожие видео

WANANCHI KIJIJI CHA MARWA -SAME, WALIA KUPORWA HEKARI ZAIDI YA ELFU MBILI(2) YA MALISHO.

WANANCHI KIJIJI CHA MARWA -SAME, WALIA KUPORWA HEKARI ZAIDI YA ELFU MBILI(2) YA MALISHO.

VITUKO VYA JOTI NA NANGA MBELE YA RAIS SAMIA,

VITUKO VYA JOTI NA NANGA MBELE YA RAIS SAMIA, "MTU WA SYSTEM"

66 миллионов лет назад: последний день динозавров

66 миллионов лет назад: последний день динозавров

Шокирующее признание Трампа / ЕС срочно меняет планы

Шокирующее признание Трампа / ЕС срочно меняет планы

Глухой депутат вошел в историю парламента, впервые выступив с речью, и его выступление было встре...

Глухой депутат вошел в историю парламента, впервые выступив с речью, и его выступление было встре...

Madereva watanzania waliotekwa Congo wasimulia ilivyotokea mpaka kuokolewa kwao

Madereva watanzania waliotekwa Congo wasimulia ilivyotokea mpaka kuokolewa kwao

Хиросима: День, когда упало небо | Многоязычный документальный фильм

Хиросима: День, когда упало небо | Многоязычный документальный фильм

#LIVE: BUNGE LA KUMI NA TATU, MKUTANO WA PILI, KIKAO CHA NANE, TAREHE 05 FEBRUARI, 2026

#LIVE: BUNGE LA KUMI NA TATU, MKUTANO WA PILI, KIKAO CHA NANE, TAREHE 05 FEBRUARI, 2026

Changamoto za madereva wa malori ya mizigo

Changamoto za madereva wa malori ya mizigo

Changamoto za madereva wa masafa marefu

Changamoto za madereva wa masafa marefu

DEREVA MTANZANIA AUAWA CONGO MBELE YA POLISI, KIONGOZI AELEZA -

DEREVA MTANZANIA AUAWA CONGO MBELE YA POLISI, KIONGOZI AELEZA - "TUNAVAMIWA SANA, HAWACHUKUI HATUA"

Usafiri wa chukudu DRC

Usafiri wa chukudu DRC

Экстренное решение Минобороны / Отвод войск?

Экстренное решение Минобороны / Отвод войск?

Haya ndio majanga yanayowakuta waendesha malori ya mizigo

Haya ndio majanga yanayowakuta waendesha malori ya mizigo

Что произошло с лидером Ливии Каддафи в последние часы перед его убийством?

Что произошло с лидером Ливии Каддафи в последние часы перед его убийством?

Взрыв у Кремля? / Теракт на Красной площади

Взрыв у Кремля? / Теракт на Красной площади

⚡️ Флот РФ ударил по Украине || Армия потеряла ключевые позиции

⚡️ Флот РФ ударил по Украине || Армия потеряла ключевые позиции

Послушайте, что Мозес Куриа сказал Руто лично в президентском дворце во время встречи кандидатов ...

Послушайте, что Мозес Куриа сказал Руто лично в президентском дворце во время встречи кандидатов ...

DEREVA MKONGWE ALIVYO KUTANA NA VIUMBE WAAJABU BARABARANI,ASIMULIA MWANZO MWISHO

DEREVA MKONGWE ALIVYO KUTANA NA VIUMBE WAAJABU BARABARANI,ASIMULIA MWANZO MWISHO

Почему Польша купила тысячу корейских танков вместо Абрамсов и Леопардов?

Почему Польша купила тысячу корейских танков вместо Абрамсов и Леопардов?

© 2025 ycliper. Все права защищены.

  • Контакты
  • О нас
  • Политика конфиденциальности

Контакты для правообладателей: [email protected]