ycliper

Популярное

Музыка Кино и Анимация Автомобили Животные Спорт Путешествия Игры Юмор

Интересные видео

2025 Сериалы Трейлеры Новости Как сделать Видеоуроки Diy своими руками

Топ запросов

смотреть а4 schoolboy runaway турецкий сериал смотреть мультфильмы эдисон
Скачать

Ukweli Kuhusu Ufugaji wa Kuku Chotara Tanzania - KUROILER

Автор: Changamkia Fursa

Загружено: 2022-02-21

Просмотров: 40457

Описание: UFUGAJI WA KUKU CHOTARA

Ufugaji wa kuku Chotara ni Ufugaji wa kibiashara na unapotaka kuanza biashara yeyote ni muhimu ukawa na mpango thabiti wa namna gani utaiendea biashara hiyo ili iweze kukuwa na kukupa mafanikio makubwa na unayoyahitaji.

Jifunze Zaidi:    • Ufugaji wa Kuku Chotara Biashara  

Biashara ya ufugaji wa kuku chotara imegawanyika katika makundi tofautitofauti, makundi hayo ni kama yafatayo:-
1. Uzalishaji wa mayai au vifaranga au vyote kwa pamoja
2. Uzalishaji wa vifaranga wa wiki 4-5
3. Uzalishaji wa kuku chotara kwaajili ya nyama
Kabla haujaanza ufugaji wa kuku chotara yakupasa uwe umechagua ni aina gani ya bidhaa unataka kuingiza sokoni. Soko kubwa la kuku chotara ni wafugaji ambao wanataka kuingia kwenye biashara hiyo, kwahiyo yakupasa mhamasishaji na uwe na ushiwishi kwa wengine ili kujitanulia soko.

Lakini zipo hatua ambazo inakubidi uzifahamu na uzipitie ili uweze kufuga kuku chotara kwa mafanikio.
Hatua hizo ni kama zifatazo:-

1. Unahitaji Kuzalisha Bidhaa ya aina gani ._
Kama nilivyotangulia kusema hapo awali kuwa ufugaji wa kuku chotara umegawanyika katika makundi tofautitofauti, unapo hitaji kuanza ufugaji wa kuku chotara unatakiwa kuchagua kundi moja na ukawekeza nguvu ya kutosha ili kuongeza thamani ya utakachozalisha.

Kundi la 1.
Uzalishaji wa mayai au vifaranga au vyote kwa pamoja.
Katika kundi hili, mfugaji wa kuku chotara anatakiwa kuwa na kuku wazazi watakao kuwa wanazalisha mayai kwaajili ya biashara, au kutotoleshe vifaranga kwaajili ya biashara au kufanya vyote kwa pamoja, kuzalisha mayai na kuuza vifaranga.
Uwekezaji kwenye kundi la kwanza unahitaji mtaji mkubwa kidogo hivyo unapaswa kujiandaa vizuri ili uweze kuwahudumia na kuwapa mazingira mazuri kuku wazazi.

Kundi la 2.
Uzalishaji wa vifaranga wa wiki 4-5
Katika kundi hili mfugaji wa kuku chotara anatakiwa kuwa na banda la kulelea vifaranga mpaka watakapo fikisha wiki 4 -5. Sio lazima kwa mfugaji kwenye kundi hili kuwa na kuku wazazi, unachotakiwa kufanya ni kutafuta wazalishaji wa vifaranga bora vya kuku chotara ambao watakuwa wakikuhudumia vifaranga kwaajili ya biashara yako.
Kitu muhimu cha kuzingatia ni kuhakikisha, vifaranga wanapata chakula bora na chanjo zote za muhimu kwa wakati.

Vilevile muwekezaji kwenye kundi la kwanza anaweza akafanya biashara hii kama atakuwa na eneo la kutosha kwa sababu wafugaji wengi wanaoanza wanaogopa kulea vifaranga wa siku moja.

Kundi la 3.
Uzalishaji wa kuku wa nyama
Katika kundi hili mfugaji wa kuku chotara anatakiwa kuwalea vifaranga mpaka watakapofiksha wiki 10-12 ambapo watakuwa tayari wamepevuka kwaajili ya nyama. Sio lazima kwa muwekezaji katika kundi hili kuwa na kuku wazazi, unachotakiwa kufanya ni kutafuta wazalishaji bora wa vifaranga vya kuku chotara atakaye kuwa anakuhudumia vifaranga kwaajili ya biashara yako.
Kitu cha kuzingatia kwenye uwekezaji huu ni kuwalisha chakula bora na ambacho hakina gharama kubwa ili uweze kupata faida.

2. Kutafuta elimu ya ufugaji wa kuku chotara._
Elimu ya ufugaji wa kuku chotara ni muhimu sana na itakupa mwanga wa utakachenda kukifanya.
Elimu hiyo ihusishe vitu vifatavyo;-

I. Ujenzi wa Banda la kuku chotara
Katika vitu ambavyo mfugaji wa kuku chotara unanatakiwa kuvizingatia ni ujenzi wa banda la kuku kwa sababu hawa kuku chotara wanaathiriwa sana na hali ya hewa inayosababishwa na mazingira ukilinganisha na kuku wa kienyeji. Wafugaji waliojenga mabanda bora wamafanikiwa kupunguza changamoto za magojwa kwa kiasi kikubwa.

II. Utaratibu wa kuwapa chanjo vifaranga
Hili halina mjadala, ili kuwakinga kuku wako dhidi ya magonjwa yasiyokuwa na tiba na ambayo husababisha vifo kwa asilimia kubwa ni kuwa na elimu ya kuwapa chanjo kwa wakati.

III. Udhibiti wa Magonjwa mbalimbali yanayosababisha vifo kwa kuku, magonjwa haya ni magonjwa ya miripuko kama typhoid, kipindupindu, coccidiosis, Coryza n.k

IV. Jinsi ya kuwalisha kuku kwenye umri tofauti ili kuhakikisha wanakuwa vizuri na wanataga mayai mengi.

V. Mbinu za kupunguza gharama za ulishaji wa chakula, mfano kuwalisha hydroponics na Azolla n.k.


3. Fahamu bajeti ya uendeshaji wa mradi._
Fanya hesabu ya kila kitu kinachohitajika ili kufahamu bajeti ya uendesgaji wa mradi, kuanzia vifaranga wanaingia bandani mpaka kufikia uzalishaji. Hesabu hiyo ihusishe vitu vifatavyo:-

I. Gharama ya ujenzi wa banda
II. Vifaa muhimu bandani
Vyombo vya chakula na maji kwenye umri tofauti, vyanzo vya joto (jiko au balb), bruda, thermometer, mkaa, maranda na magazeti
III. Chakula kwa rika tofauti
Gharama ya chakula watakachokula mpaka waanze uzalishaji
IV. Chanjo na antibiotiki
Gharama ya antibiotiki na chanjo watakazotumia mpaka kufikia uzalishaji
V. Gharama ya umeme

Sio lazima uwe na pesa yote kwa pamoja ndio uanze ufugaji wa kuku chotara, bali unaweza kuanza hata kama unarobo ya pesa inayohitajika. Kikubwa uainishe vyanzo vya pesa itakayotumika kuendeleza mradi.

#kuroiler
#chotara

Не удается загрузить Youtube-плеер. Проверьте блокировку Youtube в вашей сети.
Повторяем попытку...
Ukweli Kuhusu Ufugaji wa Kuku Chotara  Tanzania - KUROILER

Поделиться в:

Доступные форматы для скачивания:

Скачать видео

  • Информация по загрузке:

Скачать аудио

Похожие видео

Kuroiler Wanataga Mapema, Mayai 260 na Uzito wa Kilo 5

Kuroiler Wanataga Mapema, Mayai 260 na Uzito wa Kilo 5

siri ya uzoefu wa zaidi ya miaka tisa katika ufugaji wa kisasa wa kuku, Kimey farm product

siri ya uzoefu wa zaidi ya miaka tisa katika ufugaji wa kisasa wa kuku, Kimey farm product

KUKU NI PESA - KUKU WANALIPA

KUKU NI PESA - KUKU WANALIPA

Он Избил Мухаммеда Али… Майк Тайсон Отомстил!

Он Избил Мухаммеда Али… Майк Тайсон Отомстил!

MAKALA YA SHAMBANI: Somo la ufugaji wa kuku aina ya Kroila

MAKALA YA SHAMBANI: Somo la ufugaji wa kuku aina ya Kroila

Why Tanzania leads in Broiler Chicken Farming

Why Tanzania leads in Broiler Chicken Farming

#SILVERLANDS WANAKULETEA KUKU AINA YA SASSO KATIKA MAONESHO YA NANENANE   |    MBEYA

#SILVERLANDS WANAKULETEA KUKU AINA YA SASSO KATIKA MAONESHO YA NANENANE | MBEYA

KATI YA SASSO NA KROILER ANAYEFAA KWA BIASHARA YA HARAKA YA NYAMA NI SASSO

KATI YA SASSO NA KROILER ANAYEFAA KWA BIASHARA YA HARAKA YA NYAMA NI SASSO

Sikushauri Ufuge Kuku wa Mayai Kama Huna Mtaji wa Kutosha — Ukweli Mgumu Bila Kupendelewa!

Sikushauri Ufuge Kuku wa Mayai Kama Huna Mtaji wa Kutosha — Ukweli Mgumu Bila Kupendelewa!

Fahamu tofauti zilizopo kati ya kuku chotara aina ya Kuroiler na Sasso

Fahamu tofauti zilizopo kati ya kuku chotara aina ya Kuroiler na Sasso

MJUE VIZURI KUKU CHOTARA, ATAGE AU NYAMA, #ufugaji #ufugajiwakuku

MJUE VIZURI KUKU CHOTARA, ATAGE AU NYAMA, #ufugaji #ufugajiwakuku

Ufugaji wa Kuku Chotara Biashara

Ufugaji wa Kuku Chotara Biashara

WEZESHWA NA INTERCHIC

WEZESHWA NA INTERCHIC

UFUGAJI KUKU CHOTARA

UFUGAJI KUKU CHOTARA

BANDA BORA ,ENEO DOGO LINALO FUGA KUKU WENGI

BANDA BORA ,ENEO DOGO LINALO FUGA KUKU WENGI

BANDA BORA LA KUKU 1500 KEREGE BAGAMOYO

BANDA BORA LA KUKU 1500 KEREGE BAGAMOYO

Ufugaji wa Kuku Chotara Kuroiler na Sasso - Part 1

Ufugaji wa Kuku Chotara Kuroiler na Sasso - Part 1

Mswada wa Samia Kumtengua Dr.Nchimbi Makamu wa Rais Tanzania Bungeni intelijensia yatoa taarifa

Mswada wa Samia Kumtengua Dr.Nchimbi Makamu wa Rais Tanzania Bungeni intelijensia yatoa taarifa

NILIANZA NA KUKU 50 WA KIENYEJI  SASA NINAUZA VIFARANGA 2500 KILA WIKI

NILIANZA NA KUKU 50 WA KIENYEJI SASA NINAUZA VIFARANGA 2500 KILA WIKI

MFUGAJI MKURANGA AELEZEA JINSI YA KUWA BILIONEA KWA KUFUGA KUKU WA MAYAI .

MFUGAJI MKURANGA AELEZEA JINSI YA KUWA BILIONEA KWA KUFUGA KUKU WA MAYAI .

© 2025 ycliper. Все права защищены.



  • Контакты
  • О нас
  • Политика конфиденциальности



Контакты для правообладателей: [email protected]