MADIWANI SIMAMIENI MIRADI YA MAENDELEO, UKUSANYAJI MAPATO YA NDANI.
Автор: MASASI ONE ONLINE TV
Загружено: 2026-02-05
Просмотров: 88
Описание:
BARAZA la Madiwani la Halmahauri ya Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara hii leo Febuari nne 2026 limeketi kwa ajili ya kujadili na kupitia taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa robo ya pili ya mwaka 2025/2026 ikiwa ni sehemu ya wajibu wake kisheria kusimamia rasilimali za umma na utekelezaji wa miradi ya maeneleo katika Halmashauri hiyo.
Kupitia kikao hicho taarifa za kamati za kudumu za Halmahauri ziliwasilishwa na kujadiliwa kwa kina na Madiwani, huku madiwani wakitoa maoni, ushauri, kuuliza maswali na kutoa mapendekezo kwa lengo la kusimamia na kuimarisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri yao inayotekelezwa ndani ya kata zote 34 za Halmashauri ya wilaya ya Masasi,
Akifungua kikao hicho, mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Bashiru Mboneche ambaye pia ni diwani kata ya Ndanda wamewasisitiza madiwani hao kuongeza juhudi na maarifa katika kusimamia miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao sambamba na kushirikiana na wataalumu wa Halmashauri ili miradi yote inayotekeza na Halmashauri iweze kukamilika na kuleta tija kwa wananchi. Na hapa anaeleza .
Kwa upande wake,Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,Optatus Lusolela ambaye pia ni mkuu wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu Halamshauri ya wilaya ya Masasi amesema kuwa Halmashauri itaendelea kushirikiana kwa karibu na madiwani katika utekelezaji wa mipango ya Halmshauri ili kufanikisha utoaji huduma bora kwa wananchi wa Halmashauri hiyo.
Nao Madiwani wa Halmashauri hiyo hawakusita kutoa ushauri wao juu ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo afya, elimu, maji na miundombinu ya barabara.
Mweneyekiti wa Mapinduzi (CCM) wilaya ya Masasi, Mariam Kasembe ametoa msisitizo kwa watendaji wa halmashauri kusoma ilani ya chama cha mapinduzi na kuitekeleza kwa vitendo na kuwataka madiwani kusimamia mapato ya halmahauri ili halmahauri iweze kuetekeleza malengo iliyojiwekea.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: