KULIKONI IKULU ZANZIBAR CHAPCHAP KIKAO CHA VIONGOZI WAKUU NA WAJUMBE WA BARAZA LA ULAMAA ZANZIBAR
Автор: Tifu Tv
Загружено: 2024-08-23
Просмотров: 9336
Описание:
Zanzibar,
23 Ogasti, 2024
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Al hajj Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema kuna haja kwa Serikali kuangalia kwa karibu miundombinu duni ya madrasa, maslahi ya walimu wa madrasa na maimamu wa misikitini.
Al hajj Dk. Mwinyi, aliyasema hayo Ikulu, Zanzibar kwenye mazungumzo na viongozi wakuu na wajumbe wa Baraza la Ulamaa Zanzibar waliofika kumtembelea.
Amesema, miundombinu ya madrsara, maslahi ya walimu madrsara na ma imamu wa misikitini nchini ni dhaifu mno, alisema ni vyema Serikali kwa kushirikiana na vyombo vya kidini kuangalia njia nzuri ya kufanyakazi na kusaidia namna ya kuzitatua changamoto hizo.
Akizungumzia suala la mmong’onyoko wa maadili kwa jamii, Al haj Dk. Mwinyi alisifu juhudi za Baraza hilo kwa kuendelea kutoa elimu kwa jamii licha ya tatizo hilo kuwa kubwa.
Pia, Alhaj Dk. Mwinyi ameupongeza uongozi na wajumbe wa baraza hilo kwa jitihada zao za kutoa elimu ya ndoa kwa wanandoa na warajis wa ndoa kwa Unguja na Pemba ili kupunguza matatizo na migogoro ya ndoa kwenye jamii sambamba na kutoa fatwa kutokana na changamozo zinazo ikabili jamii.
Kuhusu migogoro mbalimbali inayohusiana na dini ya kiislamu kwenye jamii, Alhaj Dk. Mwinyi amelipongeza Baraza hilo kwa weledi wa utatuzi mzuri wa migogoro hiyo, sambamba na kutatua hata viashiria vinavyosababisha migogoro hiyo.
Vilevile, Alhaj Dk. Mwinyi hakuacha kulisihi Baraza hilo kuendelea kuisimamia amani na utulivu kwa kutumia lugha moja kupitia viongozi wao, maimamu misikitini pamoja na wanasiasa kwenye majukwaa yao ili kuendeleza taifa lenye umoja na mshikamano.
Naye, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaab, alipongeza juhudi za maendeleo anazozisimamia Alhaj Dk. Mwinyi hasa kwa kipindi kifupi cha uongozi wake, pia alimuahidi Al haj Dk. Mwinyi kumpa ushirikiano wa hali ya juu kutoka kwa baraza hilo kupitia misingi ya quran, hadithi, fikhi na tafsiri pamoja na kufuata miongozo na sunnah za Mtume (S.A.W) hasa kwenye suala zima la kusimamia ustawi, amani na utulivu wa nchi.
Mapema, akizungumza kwenye kikao hicho, Katibu Mtendaji kutoka Ofisi ya Mufti Zanzibar, Sheikh Khalid Ali Mfaume amesema, miongoni mwa kazi za bara hilo mbali na kumshauri na kumsaidia Mufti mkuu wa Zanzibar pia wanatoa elimu kwa walimu wa madrasa, wanandoa na warajis wa ndoa kwa kuwakabidhi vibali baada ya kuhitimu mafuzo, kutatua mambo mbalimbali ya dini ikiwemo kutoa fatwaa kwa matatizo yanayoikabili jamii.
IDARA YA MAWASILIANO IKULU, ZANZIBAR.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: