BRELA YATOA MAFUNZO KWA KLABU YA MILIKI UBUNIFU CHUO KIKUU CHA MZUMBE - MBEYA
Автор: BRELA ONLINE TV
Загружено: 2026-01-13
Просмотров: 26
Описание:
Wanafunzi wanaoongoza Klabu ya Miliki Ubunifu nchini wametakiwa kuwa mabalozi wazuri wa kusambaza elimu ya Miliki Ubunifu kwa wenzao vyuoni na katika jamii kwa ujumla, ili kuongeza uelewa na ushiriki wa vijana katika kulinda bunifu na vumbuzi zao.
Wito huo umetolewa leo tarehe 13 Januari, 2026 na Msajili Msaidizi kutoka Kurugenzi ya Miliki Ubunifu, BRELA, Bi. Neema Kitala wakati wa Mafunzo maalumu kwa viongozi wa Klabu ya Miliki Ubunifu kutoka Chuo Kikuu Mzumbe, Ndaki ya Mbeya.
Kupitia Mafunzo hayo, wanafunzi wameelimishwa juu ya faida za Miliki Ubunifu na taratibu za usajili wa Alama za Biashara na Huduma, pamoja na Hataza ili waweze kuwahamasisha wenzao chuoni kujiunga na Klabu hiyo kwa wingi zaidi na kutumia fursa zilizopo.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: