KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 05/01/2026
Автор: KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH
Загружено: 2026-01-05
Просмотров: 3815
Описание:
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 05/01/2026
UJUMBE WA LEO:"JARIBU LA KIUCHUMI".
LENGO LA SOMO:
Mungu akukupa AKILI ili apate KUFAHAMU katika:
(a) Jinsi ikupasavyo kuenenda eneo la UCHUMI katika MAJIRA tuliyonayo.
(b) Kujua cha KUOMBA na namna ya KUOMBA.
1 Wakorintho 10 : 13
Daniel 9 : 22
Zaburi 105 : 4
Luka 22 : 31 - 32
Kumbukumbu 8 : 18
Hosea 4 : 6
Warumi 10 : 1 - 2
1 Wafalme 3 : 12
Mhubiri 11 : 2
Mithali 6 : 6 - 8
Tito 3 : 14
Mungu akukupa AKILI ili apate KUFAHAMU katika:
(a) Jinsi ikupasavyo kuenenda eneo la UCHUMI katika MAJIRA tuliyonayo.
(b) Kujua cha KUOMBA na namna ya KUOMBA.
1 Wakorintho 10 : 13
13 Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.
Daniel 9 : 22
22 Akaniagiza, akaongea nami, akasema, Ee Danieli, nimetokea sasa, ili nikupe akili upate kufahamu.
Luka 22 : 31 - 32
31 Akasema, Simoni, Simoni, tazama, Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano;
32 lakini nimekuombea wewe ili imani yako isitindike; nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako.
Kumbukumbu 8 : 18
18 Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.
Hosea 4 : 6
6 Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.
Warumi 10 : 1 - 2
1 Ndugu zangu, nitakayo sana moyoni mwangu, na dua yangu nimwombayo Mungu, ni kwa ajili yao, ili waokolewe.
2 Kwa maana nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa.
1 Wafalme 3 : 12
12 basi, tazama, nimefanya kama ulivyosema. Tazama, nimekupa moyo wa hekima na wa akili; hata kabla yako hapakuwa na mtu kama wewe, wala baada yako hatainuka mtu kama wewe.
Mhubiri 11 : 2
2 Uwagawie sehemu watu saba, hata wanane; Maana hujui baa gani litakalokuwa juu ya nchi.
Mithali 6 : 6 - 8
6 Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima.
7 Kwa maana yeye hana akida, Wala msimamizi, wala mkuu,
8 Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua; Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno.
Tito 3 : 14
14 Watu wetu nao wajifunze kudumu katika matendo mema, kwa matumizi yaliyo lazima, ili wasiwe hawana matunda.
AGENDA ZA MAOMBI
1. SHUKRANI
2. Omba Neema na Msaada wa Mungu
3. Omba MAARIFA, HEKIMA NA AKILI eneo la
Uchumi katika Majira haya
Mhubiri: Mwl . Eng. Goodluck Mushi
Kwa maombi na ushauri :
Mch. Kiongozi: Dr. Eliona Kimaro
Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053
Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga
Simu: +255 713 553 443
YouTube: Kijitonyama Lutheran church
Barua Pepe : [email protected]
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: