RC HALIMA DENDEGO: WANASINGIDA KUANGALIA FAINALI BURE BOMBADIA, AWAOMBA KUOMBEA SIMBA SC
Автор: CALES TV
Загружено: 2025-05-24
Просмотров: 285
Описание:
Singida, Tanzania –
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mheshimiwa Halima Dendego, ametangaza kuwa mashabiki wa soka mkoani hapa watapata fursa ya kipekee ya kuangalia bure mchezo wa fainali ya kihistoria kupitia big screen itakayowekwa katika uwanja wa kisasa wa Bombadia uliopo mjini Singida.
Akizungumza leo na vyombo vya habari, Mheshimiwa Dendego alisema kuwa hatua hiyo inalenga kuwapa wananchi wa Singida nafasi ya kufurahia kwa pamoja mchezo huo mkubwa wa soka na kuhamasisha mshikamano wa kitaifa kupitia michezo.
“Nitaweka screen katika uwanja wa Bombadia ili Wanasingida waangalie fainali hiyo ya kihistoria nchini. Nawaomba Wanasingida tuiombee timu yetu ya Simba ili iweze kushinda na kulibakisha kombe hilo nchini,” alisema RC Dendego.
Aliongeza kuwa ushindi wa Simba utakuwa ni heshima kubwa kwa taifa na kwa viongozi wetu wakuu, akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mheshimiwa Dkt. Hussein Mwinyi.
Uwanja wa Bombadia unatarajiwa kupokea maelfu ya mashabiki siku ya fainali, huku maandalizi ya usalama na huduma muhimu yakiwa yamekamilika ili kuhakikisha tukio hilo linafanyika katika mazingira salama na yenye furaha.
Wakazi wa Singida wametakiwa kujitokeza kwa wingi, huku wakihimizwa kuvaa mavazi ya rangi za timu wanayoishabikia na kushiriki kwa amani katika kusherehekea burudani hiyo ya kipekee ya soka.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: