FAMILIA YA WATU 5 WAFARIKI KWA MKASA WA MOTO BULAPESA HUKU WAKAAZI WENYE GHADHABU WAKILIPIZA KISASI
Автор: 𝐖𝐀𝐒𝐎 𝐓𝐕
Загружено: 2025-07-16
Просмотров: 4271
Описание:
Biwi la simanzi limeghubika wakaazi wa bula pesa hii ni baada ya mkasa wa moto wa kuhuzunisha kuzuka usiku wa kuamkia jumatano huko Kachewa jimboni Isiolo ambapo watu 5 wa familia moja walipoteza maisha kutokana na moto huo.
Kulingana na ripoti za eneo hilo, moto huo ulizuka usiku wa manane familia hiyo wakiwa wamelala.
Akizungumza na wanahabari Chifu wa lokesheni ya kati Abdi Dida amesema kwamba amesikitishwa na kisa hicho na kukilaani vikali .
Chifu dida amethibitisha kwamba mshukiwa aliyetekeleza kisa hicho pia aliteketezwa na wakaazi waliokuwa na hamaki na hata kutekeketeza nyumba yake.
Afisa huyo wa utawala amesema kifungua mimba wa familia huyo alinusurika mkasa huo kwani hakuwemo wakati wa tukio.
Ametoa wito kwa wakaazi kutochukua sheria mkononi kisa kama hicho kinapotendeka.
Wakati huo huo ,Omar Godana ambaye ni mzee wa jamii ameaimiza umuhimu wa kutatua mgogoro kwa njia inayofaa ikiwa mmoja amehisi kudhulumiwa .
Hayo yakijiri , Duba Kuno ambaye alikuwa diwani amewarai wakaazi kuwa wavumilivu na watulivu katika kipindi cha msiba na maombolezi .
Inadaiwa kwamba kisa hicho kilisababishwa na mgogoro wa kimapenzi.
Join this channel to get access to perks:
/ @wasotv
WASO TV - Informing and Entertaining
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: