MKANDARASI ONYO KALI KUKAMILIKA KWA UJENZI WA CHUO CHA MZUMBE KAMPASI YA TANGA UJENZI UKAMILIKE
Автор: 17 PLUS TV
Загружено: 2025-12-30
Просмотров: 3
Описание:
Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Gilibert Kalima, amemtaka mkandarasi anayetekeleza mradi wa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Kampasi ya Tanga kuhakikisha anakamilisha ujenzi huo kwa wakati uliopangwa, akisisitiza umuhimu wa kuzingatia viwango vya ubora na ratiba ya kazi kama ilivyobainishwa kwenye mkataba.
Pamoja na hayo, Kalima ameendelea kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuboresha elimu ya juu nchini, hatua zinazolenga kuongeza fursa za elimu na maendeleo ya rasilimali watu.
Aidha, Kalima amewataka wananchi wanaoishi jirani na mradi huo kuwa walinzi wa miundombinu hiyo na kuepuka kufanya vitendo vyovyote vya uharibifu ambavyo vinaweza kukwamisha utekelezaji na ufanisi wa kazi katika eneo hilo.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: