Yaepuke Haya Kwenye Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji
Автор: Changamkia Fursa
Загружено: 2019-07-29
Просмотров: 33126
Описание:
Epuka Mambo haya kwenye ufugaji wa kuku
Ndugu mfugaji ni ukweli usiopingika wala kujadilika kuwa katika ufugaji kuna baadhi ya mambo wafugaji tunayafanya lakini hayakupaswa kufanyika,
Yafuatayo ni ya kujiepusha nayo katika ufugaji:-
1. Kuingiza kuku wageni bila kujua historia ya chanjo walipotoka.
Unapofanya kitendo hicho basi ujue fika kwamba kuna uezekanao mkubwa wa kuleta magonjwa katika kuku wako, hivyo unashauriwa kwamba usiwachanganye kuku wako na kuku wengine wapya ili kuepusha magonjwa kwa kuku wako walikuwapo bandani.
2. Kutibu kwa mazoea bila kuwasiliana na Afisa Mifugo.
3. Kutembelea mabanda ya jirani bila kuchukua tahadhari.
4. Kutupa kuku waliokufa porini.
5. Kuacha banda chafu,
Yapo magonjwa mengi ya kuku ambayo chanzo chake kikubwa ni uchafu unaotokana na kuku wenyewe, vitu kama vile chakula kilichokaa muda mrefu bila kuliwa na kuku wenyewe, kinyesi cha kuku na uchafu mwingine ukikaa bandani ,muda mrefu pasipo kutolewa huwa na madhara makubwa sana kataika ufugaji wa kuku.
6. Kuuza/ kuchinja kuku wagonjwa,
Bila shaka utakuwa umekuwa ukiona wengi wanauza kuku wao kwa sababu wameugua. Lakini ukweli ni kwamba tunashauriwa na watalamu wa kilimo na ufugaji ya kwamba tusipendelee kuwauza kuku ambao ni wagonjwa kwa sababu hatujui madhara yatakayompata mlaji wa kuku mara baada ya kula nyama ya kuku ambayo chanzo chake ilikuwa ni ugonjwa.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: