WABUNGE WAWILI WABURUZWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA RUSHWA CHATO.
Автор: NYOTARAYS TV
Загружено: 2026-03-10
Просмотров: 68
Описание:
Taasisi ya Kuzuia na Kupanda na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Geita imewapandisha mahakamani, Mbunge wa Jimbo la Chato Kasikazini Paschal Lutandula pamoja na Mbunge wa Jimbo la Chato Kusini Mh. Cornel Magembe wote wakituhumiwa kujihusisha na Vitendo vya Rushwa kwa Nyakati Tofauti.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Geita James Ruge amesema Mbunge Cornel Magembe Kwa kushirikiana na Frank Francis ambaye ni Diwani Kata ya Mganza wanatuhumiwa kwa kukusanya Madiwani wateule 20 wa Halmashauri ya wilaya ya Chato kwa lengo la kuwashawishi kwa hongo ya Fedha , chakula na Malazi ili kupiga kura za upendeleo katika uchaguzi wa ndani kumpata Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato.
Aidha amesema Mbunge wa Jimbo la Chato Kusini, Mh Paschal Lutandula kwa kushirikiana na Bartholomeo Manunga aliyekuwa Diwani Kata ya Bwongera na Josephat Elias aliyekuwa Diwani Kata ya Bwera katika kuwania nafasi ya mwenyekiti wa halmashauri walituhumiwa kujenga ushawishi wenye vitendo vya rushwa kwa Diwani wa Kata ya Muungano Njile Charles kwa kumpa hongo ili kujiondoa katika kinyang’anyiro cha uchaguzi ili kumpatia ushindi wa wazi ndgu Bartholomeo Manunga katika uchaguzi huo.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: