Historia ya Mzozo wa Palestine na Israel
Автор: TRT Afrika Swahili
Загружено: 2023-10-16
Просмотров: 2745
Описание:
Mzozo wa Palestine na Israel ni wa muda mrefu kuwahi kutokea duniani, ambao umeanza mwanzoni mwa miaka ya 1900, ambapo kundi dogo la Mayahudi Wazungu walipotaka kuanzishwa kwa makazi ya Mayahudi.
Mwaka 1917, aliyekuwa wakati huo, waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, Arthur Balfour, aliandika barua kwa Lionel Walter Rothschild, kiongozi wa jamii ya Mayahudi wa Uingereza.
Katika barua hiyo, Balfour alionyesha dhamira ya serikali ya uingereza ya kusaidia “kuanzishwa kwa makazi ya mayahudi katika eneo la Palestine.”
Barua hiyo, tangu enzi, imekuwa ikijulikana kama Makubaliano ya Balfour. Mnamo mwaka 1922, Umoja ya Mataifa ya wakati huo ambayo ilikuwa ikifahamika kama ‘The League of Nations’ iliipa Uingereza mamlaka ya kutawala eneo ambalo wakati huo liliitwa Palestine.
Ambayo leo hii, ni Israel pamoja na Ukingo wa Magharibi na Gaza.
Wakati wa utawala huo, Uingereza iliruhusu wimbi la wahamiaji wa kiyahudi kuingia Palestine na kuanza kutimiza malengo ya kuanzishwa kwa taifa ya kiyahudi katika ardhi ya Palestine.
Uhamiaji wa Wayahudi katika ardhi ya Palestine kati ya vurugu za mara kwa mara kati ya mayahudi na waaarabu.
Mwezi Mei, tarehe 14, 1948, Uingereza ilimaliza utawala wake Palestine kufuatia makubaliano ya Umoja wa Mataifa ya mwaka wa 1947, ambayo yalitaka kugawanywa kwa eneo hilo kati ya Waarabu na Wayahudi.
Siku hiyo hiyo, taifa la Israel liliundwa kwa eneo lililopewa Wayahudi kwa mujibu wa Mpango wa kuligawa.
#habari #Gaza #historia
Fuatilia Habari zetu:
🌐 https://www.trtafrika.com/sw
Tiktok
🟣 / trtafrikasw
Facebook
🔵 / trtafrikasw
Youtube
🔴 / @trtafrikasw
X
⚫ https://x.com/trtafrikaSW
Instagram
🟣 / trtafrikasw
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: