SKULI YA BENBELA GIRLS YAVAMIA MJI MKONGWE
Автор: ASAM Online TV
Загружено: 2026-02-16
Просмотров: 1637
Описание:
Wanafunzi wa Skuli ya Mbenbela Girls iliyopo Mjini wamehimizwa kujifunza na kuelewa historia ya Zanzibar kwa kutembelea maeneo ya hifadhi ya Mji Mkongwe pamoja na majengo yake ya kale yenye urithi mkubwa wa kihistoria.
Mafunzo hayo ni muendelezo wa ziara za kielimu zinazolenga kukuza uelewa wa wanafunzi kuhusu uhifadhi wa Mji Mkongwe na majengo ya kale. Mafunzo yaliwasilishwa na Saleh Juma Makake, Afisa Elimu kutoka Mamlaka ya Hifadhi na Uendelezaji wa Mji Mkongwe, ambaye alieleza umuhimu wa kizazi cha sasa kuutambua na kuuenzi urithi wa kihistoria.
Kwa upande wake, Bi. Zuhuru Ali Juma, Msimamizi Mkuu wa Makaburi ya Mafalme na Makumbusho, amesema ni muhimu kwa walimu kuwapeleka wanafunzi katika maeneo ya kihistoria ili wajifunze kwa vitendo badala ya nadharia pekee.
Nao wanafunzi walioshiriki mafunzo hayo wamesema wamepata maarifa mapya kuhusu historia ya Mji Mkongwe, thamani ya majengo ya kale na wajibu wao katika kuyahifadhi. Wameahidi kuendelea kutembelea maeneo ya kihistoria ili kuongeza uelewa wao na kuwa mabalozi wa uhifadhi wa urithi wa Zanzibar.
#MbenbelaGirls #MjiMkongwe #HistoriaYaZanzibar #ElimuKwaVitendo #AsamOnlineTV
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: