NINJA ATOA NENO ZITO KUAGWA KWAKE
Автор: Ctv tz online
Загружено: 2019-07-16
Просмотров: 13084
Описание:
Ctv tz online
ASHA GWARA
Katika sherehe za kumuaga aliekua mchezaji wa timu ya dar es salam young africa na timu ya taifa ya znz, zanzibar heroes abdallah shaibu (ninja) ameshauriwa na mkuu wa mkoa mjini magharibi ayoub moh'd mahmoud kujituma na kuendeleza nidhamu aliokuwa nayo ili kupata mafanikio zaidi ktk maisha yake ya soka na kuliletea heshima zaidi taifa.
Ushauri huo amepewa katika sherehe hizo zilizofanyika ktk uwanja wa amani ambapo maefu ya wazanzibar wamejitokeza kumuunga mkono mchezaji huyo pamoja na kumuombea dua ya kumtakia mafanikio ktk safari yake hio.
Nae abdallah shaibu (ninja) amewashukuru ,viongozi wa zff, viongozi wa timu yake ya yanga na mashabiki waliojitokeza ktk maagano hayo pamoja na kuwaahidi kujituma ili kutengeneza nafasi kwa wachezaji wengine.
Mchezaji huyo ameagwa rasmini siku ya jana katika kiwanja cha amani kwa kucheza michezo miwili tofauti ambapo mchezo wa awali ulikuwa ni kati ya timu ya mimi na wewe foundation dhidi ya wasanii wa kizazi kipya znz mchezo ambao umeisha kwa timu ya mimi na wewe ilioongozwa na mkuu wa mkoa ambae alikua nahodha wa timu hio imeshinda magoli matatu kwa moja dhidi ya timu ya wasanii wa kizazi kipya.
Mchezo wa pili ulikua ni kati ya timu ninja dhidi ya timu hilika ambapo timu hilika imeshinda magoli mawili kwa sifuri magoli yaliofungwa na mchezaji ambae alitoe benchi abubakar kabela katika kipindi cha pili cha mchezo huo.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: