TUZIFAHAMU NYIMBO ZETU || TMW 75 Mikononi Mwa Mitume
Автор: KKKT
Загружено: 2025-10-16
Просмотров: 248
Описание:
Wimbo huu umetungwa na Mch. Sila F. Msangi (1918–1964); anaheshimika kwa mchango wake katika nyimbo za kiswahili, hasa katika kitabu cha TMW. Miongoni mwa nyimbo zake zilizovuma ni pamoja na; Nikishika Njia Naona Mbali, Haleluya Mataifa Yote Msifuni Bwana, na Tukutane Kila Upande.
Urithi wake wa kimuziki unaendelea kuathiri muziki wa kisasa wa Kanisa, huku nyimbo zake zikiwa bado zikiimbwa na kuthaminiwa katika ibada hasa za Kilutheri. Baadaye, mwanawe ambaye pia ni Mchungaji, Herbert S. Msangi, akazitungia ala nyimbo za baba yake, akihifadhi na kukuza zaidi urithi huu wa muziki.
Karibuni tusikilize Wimbo huu MIKONONI MWA MITUME (TMW 75). Katika ibada ya kuwekwa wakfu Mch. Dk. Daniel Mono kuwa Askofu wa Dayosisi ya Mwanga, wimbo huu uliimbwa kuashiria kwamba kazi anayoiendea ni mwendelezo wa kazi za Mitume wetu, mababa wa Imani.
Mikononi mwa Mitume kazi ilifanywa; Nenda kazini na usiache Kuyasema
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: