ycliper

Популярное

Музыка Кино и Анимация Автомобили Животные Спорт Путешествия Игры Юмор

Интересные видео

2025 Сериалы Трейлеры Новости Как сделать Видеоуроки Diy своими руками

Топ запросов

смотреть а4 schoolboy runaway турецкий сериал смотреть мультфильмы эдисон
Скачать

15 WAPOTEZA MAISHA AJALI YA NDEGE YA JESHI…

Автор: Mwananchi Digital

Загружено: 2026-02-28

Просмотров: 81

Описание: Bolivia. Watu wasiopungua 15 wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa baada ya ndege ya mizigo ya Jeshi la Anga la Bolivia kuanguka katika mji wa El Alto, magharibi mwa nchi hiyo, ajali hiyo ilitokea majira ya saa 12:15 siku ya Ijumaa, ndege hiyo ilikuwa ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa El Alto ikitokea Santa Cruz, kwa mujibu wa maofisa wa usafiri wa anga.

Wizara ya Ulinzi ya Bolivia ilithibitisha kuwa ndege iliyohusika ni aina ya C-130 Hercules iliyokuwa ikisafirisha noti za fedha kwenda Benki Kuu ya Bolivia, Kamanda wa Jeshi la Anga, Sergio Lora, alisema watu wanane walikuwa ndani ya ndege hiyo wakiwemo wahudumu wa mizigo na marubani, ripoti zinasema ndege iliteleza nje ya barabara ya kurukia na kugonga magari yaliyokuwa karibu.

Shirika la habari BBC limeripoti kuwa, baada ya ajali hiyo, polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya watu waliodaiwa kujaribu kuiba noti za fedha zilizokuwa zimetapakaa eneo la tukio, video zilizosambaa zilionyesha watu wakikimbia huku maofisa wa polisi wakiwa wamejipanga kwa ngao wakidhibiti hali, baadhi ya watu walionekana wakirusha mawe katika vurugu hizo.

Chama cha Waandishi wa Habari cha Bolivia kililaani mashambulizi dhidi ya wanahabari waliokuwa wakiripoti tukio hilo, katika taarifa yake, chama hicho kilisema baadhi ya watu walishambulia vyombo vya habari kwa fujo wakijaribu kupora fedha hizo, gari la matangazo ya moja kwa moja lililengwa moja kwa moja na wanahabari kadhaa kujeruhiwa vibaya kwa kupigwa mawe.

Shirika la Habari la Serikali ya Bolivia liliripoti kuwa watu wasiopungua 12 walikamatwa kwa tuhuma za kuiba noti hizo, huku Waziri wa Ulinzi, Marcelo Salinas, alionya kuwa fedha hizo hazina thamani ya kisheria kwa kuwa hazikuwa zimetolewa rasmi na Benki Kuu wala hazina namba za usajili, na kusema kuwa yeyote atakayejaribu kuzitumia atakuwa anatenda kosa la jinai.

Wizara ya Afya ya Bolivia ilisema watu 31 walijeruhiwa katika ajali hiyo na kutoa wito wa haraka wa uchangiaji damu, Uwanja wa Ndege wa El Alto ulifungwa kwa muda kufuatia tukio hilo huku uchunguzi ukiendelea kubaini chanzo cha ajali, pia
Mamlaka zilisema matokeo ya uchunguzi yatatangazwa mara yatakapokamilika.

Shuhuda mmoja aliambia shirika la habari la Reuters kuwa dada yake alijeruhiwa baada ya tairi la ndege kuangukia gari lao wakati wa ajali, walimkimbiza hospitalini mara moja kwa matibabu baada ya kuumia kichwani kutokana na athari ya tukio hilo, magari kadhaa yaliharibiwa vibaya katika eneo la ajali.

Baadhi ya mashuhuda walidai kuwa hali ya hewa ilikuwa mbaya wakati ndege hiyo ikianguka, wakitaja mvua kubwa ya mawe na radi kali, mwanamke mmoja aliyeathiriwa alisema radi zilikuwa zikimulika angani wakati mabaki ya ndege yalipoangukia gari lake, Mamlaka zimeanzisha uchunguzi rasmi kubaini chanzo halisi cha ajali hiyo.

IMEANDALIWA NA HELLEN MDINDA KWA MSAADA WA MASHIRIKA YA HABARI.

Не удается загрузить Youtube-плеер. Проверьте блокировку Youtube в вашей сети.
Повторяем попытку...
15 WAPOTEZA MAISHA AJALI YA NDEGE YA JESHI…

Поделиться в:

Доступные форматы для скачивания:

Скачать видео

  • Информация по загрузке:

Скачать аудио

Похожие видео

США начали военную операцию против Ирана. Какая цель Трампа?

США начали военную операцию против Ирана. Какая цель Трампа?

Епископ Мчамунгу объясняет причины смерти кардинала Пенго и приводит его биографию.

Епископ Мчамунгу объясняет причины смерти кардинала Пенго и приводит его биографию.

LIVE: KUMEKUCHA DABI YANGA/SIMBA  KESHO/ TFF AFCON 2027 NI KUFURU/KIMATAIFA LIGI ZASHIKA KASI

LIVE: KUMEKUCHA DABI YANGA/SIMBA KESHO/ TFF AFCON 2027 NI KUFURU/KIMATAIFA LIGI ZASHIKA KASI

США и Израиль ударили по Ирану. Что происходит?

США и Израиль ударили по Ирану. Что происходит?

To miały być zwykłe obiady… NIE BYŁY! 😳 / Oddaszfartucha

To miały być zwykłe obiady… NIE BYŁY! 😳 / Oddaszfartucha

OSKAR Z GOLEM W PIERWSZEJ MINUCIE MECZU! CHŁOPAK ZE ZŁOTA WCHODZI Z BUTA DO PIERWSZEGO SKŁADU PORTO

OSKAR Z GOLEM W PIERWSZEJ MINUCIE MECZU! CHŁOPAK ZE ZŁOTA WCHODZI Z BUTA DO PIERWSZEGO SKŁADU PORTO

Inside Tanzania’s economic reset

Inside Tanzania’s economic reset

Ізраїль атакував Іран за підтримки США | Чи втрутиться Росія? | Навіщо це Трампу?

Ізраїль атакував Іран за підтримки США | Чи втрутиться Росія? | Навіщо це Трампу?

The Rising Woman 2026 Executive Podcast with Absa Bank Tanzania

The Rising Woman 2026 Executive Podcast with Absa Bank Tanzania

ქრონიკა 14:00 საათზე - 28 თებერვალი, 2026 წელი

ქრონიკა 14:00 საათზე - 28 თებერვალი, 2026 წელი

Analiza izraelsko-amerykańskiego ataku na Iran

Analiza izraelsko-amerykańskiego ataku na Iran

🤯ПОРТНИКОВ: Ми вже у СВІТОВІЙ війні! Ось чому почались ПЕРЕГОВОРИ

🤯ПОРТНИКОВ: Ми вже у СВІТОВІЙ війні! Ось чому почались ПЕРЕГОВОРИ

🔴LIVE: MAZISHI YA MWADWAMA POLYCARP KARDINALI PENGO MUDA HUU

🔴LIVE: MAZISHI YA MWADWAMA POLYCARP KARDINALI PENGO MUDA HUU

Nóż bushcraftowy wart 400 zł w Biedronce?

Nóż bushcraftowy wart 400 zł w Biedronce?

Jak DROGÓWKA naciąga Polaków! (I jak legalnie się bronić)

Jak DROGÓWKA naciąga Polaków! (I jak legalnie się bronić)

LIVE: US & Israel strike Iran | BBC News

LIVE: US & Israel strike Iran | BBC News

Wojna USA - Iran. Dlaczego doszło do ataku? Relacja z Waszyngtonu, co dzieje się w Teheranie?

Wojna USA - Iran. Dlaczego doszło do ataku? Relacja z Waszyngtonu, co dzieje się w Teheranie?

Депутат СЕВЕРНОГО ТУНДУРУ ОБЕЩАЕТ КРУПНЫЕ ИЗМЕНЕНИЯ ИНФРАСТРУКТУРЫ В ОКРУГЕ МАТЕМАНГА

Депутат СЕВЕРНОГО ТУНДУРУ ОБЕЩАЕТ КРУПНЫЕ ИЗМЕНЕНИЯ ИНФРАСТРУКТУРЫ В ОКРУГЕ МАТЕМАНГА

TRAMU YAPINDUKA, WAWILI WAPOTEZA MAISHA

TRAMU YAPINDUKA, WAWILI WAPOTEZA MAISHA

SZALONE DERBY TRÓJMIASTA! ŚWIETNE GOLE I NIESAMOWITA INTERWENCJA! ARKA - LECHIA, SKRÓT MECZU

SZALONE DERBY TRÓJMIASTA! ŚWIETNE GOLE I NIESAMOWITA INTERWENCJA! ARKA - LECHIA, SKRÓT MECZU

© 2025 ycliper. Все права защищены.

  • Контакты
  • О нас
  • Политика конфиденциальности

Контакты для правообладателей: [email protected]