Upendo wa Kwanza - WORSHIP SONG
Автор: Danuse Praise and Worship
Загружено: 2026-03-08
Просмотров: 67
Описание:
Ulipita kati ya makanisa saba,
Ewe Bwana Yesu uliye hai milele.
Wajua kazi zetu na saburi yetu,
Ujyaona machozi na juhudi zetu.
Lakini wasema kwa sauti ya upendo:
“Nina neno juu yako ewe kanisa langu,
Umeacha upendo wako wa kwanza,
Uwo wakiungua kama moto wa mwanzo.”
Kiitikio:
Rudi, rudi kwenye upendo wa kwanza,
Rudi moyoni mwa Bwana wako.
Tubu leo, ufungue moyo wako,
Yesu anakuita urudi kwake.
Umetenda mema na kupigana vita,
Umekataa uovu na mafundisho ya uongo.
Lakini moyo wangu watamani sana,
Upendo wako uwe moto tena.
Yeye asemaye: “Ninajua mateso yako,
Ninajua imani yako katika giza.
Usiogope yale yatakayokuja,
Uwe mwaminifu hata kufa.”
Kiitikio:
Rudi, rudi kwenye upendo wa kwanza,
Rudi moyoni mwa Bwana wako.
Tubu leo, ufungue moyo wako,
Yesu anakuita urudi kwake.
Atakayeshinda atapewa uzima,
Kula matunda ya mti wa uzima.
Atakayeshinda hatadhuriwa,
Na mauti ya pili kamwe.
Sikia sauti ya Roho Mtakatifu,
Kwa makanisa yote duniani:
Aliye na sikio na asikie leo,
Bwana anaita turudi kwake.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: