ILANI MPYA CCM YA 2025-2030 KUZALISHA AJIRA MILIONI NANE
Автор: Mwananchi Digital
Загружено: 2025-05-30
Просмотров: 931
Описание:
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Ilani yake ya Uchaguzi ya mwaka 2025-2030 kimetangaza mpango wa kuzalisha ajira zenye tija zisizopungua milioni nane katika kipindi cha miaka mitano ijayo, likiwa ni mojawapo ya vipaumbele vya kukuza uchumi na kuinua kipato cha wananchi.
Akizungumza leo Ijumaa Mei 30, 2025 wakati wa kuwasilisha vipengele vya Ilani hiyo mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM unaoendelea jijini Dodoma, Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi wa Ilani hiyo, Profesa Kitila Mkumbo amesema nusu ya ajira hizo zinalengwa kuzalishwa katika sekta rasmi.
“Katika kufanikisha lengo hili, Ilani imeainisha hatua 11 za utekelezaji ikiwamo kuanzisha programu maalum ya ujenzi wa viwanda vidogo na vya kati vya kuongeza thamani ya mazao katika kila mkoa na wilaya,” amesema Profesa Kitila.
Ameongeza kuwa CCM imedhamiria kuwawezesha wabunifu wanaoanzisha kampuni changa kwa kuwapatia mitaji ya kuanzia, hatua ambayo inalenga kuimarisha uchumi wa ubunifu na kuongeza nafasi za ajira kwa vijana.
Prof. Kitila amesema pia kwamba katika kuwaandaa vijana kushindana kwenye soko la ajira la kimataifa, Serikali ya CCM itaanzisha vituo maalumu vya mafunzo ya stadi kwa ajili ya kuwaandaa kupata ajira nje ya nchi.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: