NIDA yazindua namba maalum 15274; Wananchi kupata taarifa za NIN Bure kupitia Simu.
Автор: Nukta TV
Загружено: 2025-12-29
Просмотров: 392
Описание:
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imezindua namba maalumu (Short Code) 15274 inayomwezesha mwombaji kufahamu namba ya utambulisho wa taifa (NIN) na kujua kama kitambulisho kimechapishwa na kipo wapi, kwa kutumia simu ya mkononi bila malipo.
Uzinduzi wa huduma hiyo umefanyika Desemba 29, 2025, ambapo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, ameipongeza NIDA kwa kuendelea kubuni mifumo ya kisasa inayolenga kurahisisha utoaji wa huduma za utambulisho wa taifa kwa wananchi.
“Ninaipongeza sana NIDA kwa jitihada zake za kuendelea kubuni mifumo ya kisasa inayomlenga mwananchi moja kwa moja. Mfumo huu wa SMS ni hatua muhimu katika safari ya mageuzi ya utoaji wa huduma za vitambulisho vya taifa na namba ya utambulisho wa taifa (NIN),” alisema Waziri Simbachawene.
Ameeleza kuwa huduma hiyo mpya inaunganisha na kuimarisha mifumo mingine ya awali ikiwemo Mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao, mfumo wa makusanyo ya maduhuli, mfumo wa ushirikishanaji wa taarifa (Data Sharing) pamoja na mifumo ya usajili inayotumika katika ofisi za Wilaya, ambayo kwa pamoja imeleta mapinduzi makubwa katika utoaji wa huduma.
Aliongeza kuwa utoaji wa huduma hiyo bila malipo ni kielelezo cha dhamira ya Serikali ya kuhakikisha huduma za msingi zinawafikia wananchi wote kwa usawa, hatua iliyopunguza gharama kwa mwananchi na kusogeza huduma za Utambulisho wa Taifa karibu zaidi na jamii.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: