005-Kwanini Wailaya ya TATU kwa dhehebu zingine!!!
Автор: Hujjatul-Isalam wal-muslimin Salim Mwega
Загружено: 2026-02-24
Просмотров: 5
Описание:
5) Basi kwa nini kwenye madhebu ya kiislamu hakutajwi huyu walii wa tatu?
Jawabu:
وَمَن يَتَوَلَّ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ فَإِنَّ حِزْبَ ٱللَّهِ هُمُ ٱلْغَٰلِبُونَ
(Na atakaye mfanya Walii (atakayemtawalisha) Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walio amini, basi hakika kundi la Mwenyezi Mungu ndilo lenye kushinda.)(Al-Maida/ 56)
Hii aya inatwambia kuwa asiyewatawalisha hawa Mawalii, basi yeye sio katika kundi la Mwenyezi Mungu.lakini inaskitisha kuwa waislamu wengi walizichukua Nguzo nne zilizo tangulia na kupunguza Nguzo ya tano, ya Walii. Walipuuza Walii huyu wa tatu. Na ndiye anayekamilisha dini, na aliye nadiwa sana katika siku ya Ghadir Khum.
عن أبي جعفر عليه السلام قال: بني الإسلام على خمس: على الصلاة والزكاة والصوم والحج والولاية، ولم يناد بشيء كما نودي بالولاية، فأخذ الناس بأربع، وتركوا هذه ـ يعني الولاية ـ[3].
(Imepokelewa kutoka kwa Abu Ja'afar, (a.s.), ya kwamba amesema: Uislamu umejengeka juu ya (Nguzo) tano: juu ya swala, zaka, saumu, kuhiji na Wilaya. Na hakikunadiwa chochote kama Wilaya ilivyo nadiwa.Lakini watu wakachukua vinne, na kuliacha hili – yaani Wilaya.)(Al-Kafi: Juzuu ya 2, uk.18 na 21, Hadithi ya 3, 7 na 1.).
عن أبي جعفر عليه السلام قال: بني الإسلام على خمس: الصلاة والزكاة والصوم والحج والولاية، ولم يناد بشيء ما نودي بالولاية يوم الغدير
(Imepokelewa kutoka kwa Abu Ja'afar, (a.s), amesema: Uislamu umejengeka juu ya (Nguzo) tano: Swala, Zaka, Saumu, Hijja, na Wilaya. Na hakikunadiwa chochote kama Wilaya ilivyo nadiwa katika Siku ya al-Ghadir.( Al-Kafi: Babu: Da'aim al-Islam, juzuu ya 2, uk.21, Hadithi ya 8.)
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: