MAAGIZO YA DC BOMBOKO KWA WAMILIKI WA MABASI WANAOKIUKA SHERIA NA KUTOTUMIA STENDI KUU YA MAGUFULI
Автор: UBUNGO MANISPAA
Загружено: 2025-01-09
Просмотров: 1068
Описание:
MKUU wa wilaya ya ubungo Mhe. Hassan Bomboko amewataka wamiliki wa mabasi yaendayo mikoani wanaopakia na kushusha abiria kwenye vituo visivyo rasmi kurejea katika Stendi kuu ya mabasi ya Magufuli kama sheria inavyoelekeza.
Ameyasema hayo leo Januari 9, 2025 wakati alipotembelea na kukagua maeneo mbalimbali ya kituo hicho na kusikiliza kero za wafanyabiashara, wadau na wananchi ambao wanafanya kazi zao katika kituo hicho.
Mh. Bomboko amesema Stendi rasmi ya mabasi yanayotokea Dar es salaam kwenda mikoani ni Stendi ya Magufuli na serikali haijatoa kibali chochote na haizitambui Stendi ambazo sio rasmi, hivyo amewataka wamiliki wote wa makampuni ya mabasi kuhakikisha mabasi yao yanafata Sheria ya kutumia kituo cha mabasi cha Magufuli na waache kutumia zisizo rasmi.
Ameongeza kuwa kuanzia siku ya kesho (10 Januari, 2025) yeye na timu yake ya ulinzi na usalama atatembelea Stendi bubu zote ili kuhakikisha makampuni yote ya usafirishaji yanafata Sheria ya kurudisha shughuli zao za usafirishaji katika Stendi rasmi ya Magufuli.
Katika kuhakikisha agizo hilo linaanza kutekelezwa, Mhe. Bomboko amewataka LATRA kuhakikisha kuanzia kesho (10 Januari, 2025) mabasi yote yaanze kuingia ndani ya Stendi rasmi ya Magufuli na si vinginevyo.
Naye mwakilishi kutoka RATRA Ndg. Nziku amesema Stendi nyingine inayotambulika ni ile ya mbagara Kwa magari yanayofanya safari zake za kuelekea kusini na amekiri kuwa hizo nyingine ambazo ni kama shekilango,urafiki na nyinginezo si Stendi rasmi.
Sambamba na hayo Mhe. Bomboko amesema Serikali ina mikakati ya kujenga soko maalum kwa ajili ya wamachinga na ameahidi kuwa serikali itafanyia kazi na kutatua changamoto zote ambazo wadau hao wameziwasilisha.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: