Nuru ya Mashariki 04.03.2026
Автор: TV47 Kenya
Загружено: 2026-03-04
Просмотров: 15
Описание:
///
China yaendelea kuimarisha mafanikio ya kuondoa umaskini huku ikizidisha ushirikiano wa kitaifa
///
Mabadiliko yanayowalenga watu yanabadilisha jamii jijiniChengdu
///
Sherehe za tamaduni zang’aa china wakati wa sikukuu ya taa
///
China imepata mafanikio makubwa katika kurejesha na kuimarisha idadi ya wanyamapori adimu na walio hatarini kutoweka, kupitia mfumo wa kitaifa wa uhifadhi wa viumbe katika makazi yao ya asili, huku hifadhi za taifa zikichukua nafasi ya kipekee na matumizi ya teknolojia ya kisasa kama akili bandia (AI) yakiongezeka.Simiyu Wanjala anaarifu zaidi.
///
China imesema inaendelea kuimarisha na kupanua mafanikio yake katika kupunguza umaskini huku ikihakikisha hakuna kurejea katika hali ya umaskini.
Kauli hiyo imetolewa na msemaji wa kamati ya kitaifa ya Chinese Peoples Political Consultative Conference CPPCC liu Jieyi jijini Beijing kama asnavyoarifu Simiyu Wanjala.
///
Shughuli za kitamaduni zilijaa shamrashamra kote China Jumanne katika maadhimisho ya Tamasha la Taa za Taa tukio linaloashiria umoja, matumaini na kilele cha sherehe za Mwaka Mpya wa Kichina. Maelfu ya wakazi na watalii walishiriki katika matamasha yaliyounganisha urithi wa kale na ubunifu wa kisasa.
///
Katika ulimwengu unaokua kwa kasi, miji mingi hukimbilia maendeleo ya miundombinu na ukuaji wa uchumi. Hata hivyo, jiji la Chengdu, mwelekeo ni tofauti: maendeleo yanaanzia kwa watu. Kwa kuweka mahitaji, ustawi na sauti za wakazi wake mbele kama anavyoripoti Ronald Mutie.
///
Mkurugenzi wa maonyesho ya droni ameisaidia kubadilisha anga za usiku ambazo tayari zinang’aa katika jiji kuu la kusini-magharibi mwa China la Chongqing kuwa turubai hai ya mwanga na teknolojia, akitoa onesho la kuvutia angani ambalo limekuwa kivutio kisichokosekana kwa wageni.
Khamis Darwesh anaripoti.
///
Ifahamu China
Mauzo ya pikipiki na baiskeli za umeme kutoka mji wa Wuxi, mkoani Jiangsu mashariki mwa China, yameongezeka kwa kasi katika miaka ya hivi karibuni, yakichochewa na upanuzi wa masoko ya kimataifa na matumizi ya teknolojia za ubunifu zilizotengenezwa China. Zakia Peng anatufahamisha zaidi kwenye sehemu yetu ya Ifahamu China
///
Jifunze Kichina
Naam, mtazamaji, sasa ni wakati wa sehemu yetu ya Jifunze Kichina! Katika sehemu hii, tunawaletea masomo ya lugha ya Kichina, hatua kwa hatua, kwa njia rahisi na ya kuvutia. Karibu tujifunze pamoja.
Thank you for watching this video. Kindly subscribe for more content from 'Home of The Untold Stories.'
About TV47
'TV47 is on GOtv (Channel 102), DStv (Channel 268), SIGNET, Gotv, BAMBA and STARTIMES.
__
For Breaking News, kindly subscribe by sending ‘NEWS’ to 22047.
__
Connect with us:
Website: https://www.tv47.digital/
Facebook: / tv47ke
Twitter: / tv47news
Instagram: / tv47ke
TikTok: / tv47_ke
Telegram: https://t.me/tv47_ke
WhatsApp: 0797 047 047
__
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: