NAIBU KATIBU MKUU CCM BARA AAGIZA KUKAMILISHWA HARAKA MRADI WA SOKO KUU LA MANISPAA YA SHINYANGA.
Автор: MISALABA MEDIA
Загружено: 2026-02-02
Просмотров: 32
Описание:
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Ndg. John Mongella, ameielekeza Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kuhakikisha inakamilisha kwa haraka ujenzi wa Soko Kuu la Manispaa ya Shinyanga, mradi unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.8, ili kuwaondolea wafanyabiashara adha ya kufanya biashara nje ya soko hilo.
Ndg. Mongella ametoa maelekezo hayo leo Februari 02, 2026, wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi katika kuelekea maadhimisho ya miaka 49 tangu kuanzishwa kwa chama hicho. Amesisitiza kuwa kukamilika kwa soko hilo ni jambo la msingi katika kuboresha mazingira ya biashara, kuongeza kipato cha wafanyabiashara na kukuza mapato ya Halmashauri.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Mhe. Wakili Julius Mtatiro, amesema Serikali ya Wilaya inatambua umuhimu wa kuboresha mazingira ya biashara kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati. Amesema tayari amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga kwa lengo la kumshauri kuomba vibali husika pamoja na kutafuta wawekezaji ili kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa haraka na kuanza kutoa huduma kwa wananchi kwa wakati.
Awali, akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa vibanda 106 vya biashara, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Ndg. Michael Makotwe, amesema mradi huo umekumbwa na changamoto kadhaa, ikiwemo upatikanaji wa malighafi za ujenzi hususan mawe ya kujazia msingi, ambayo hupatikana umbali mrefu na hivyo kusababisha ucheleweshaji wa utekelezaji wa kazi.
Kukamilika kwa ujenzi wa Soko Kuu la Manispaa ya Shinyanga kunatarajiwa kuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi kwa wafanyabiashara na wananchi wa Manispaa ya Shinyanga kwa ujumla, sambamba na kuimarisha mpangilio mzuri wa shughuli za kibiashara ndani ya Manispaa.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: