Uvamizi Nchini Venezuela: Miji Kadhaa Yashambuliwa, Makomando wa Marekani Wamkamata Rais Maduro
Автор: The Chanzo
Загружено: 2026-01-03
Просмотров: 32743
Описание:
Taarifa ya kukamatwa kwa Maduro inakuja katika muda ambao serikali ya Venezuela imetangaza hali ya hatari na kuwataka wananchi kutoka nje kupinga kinachoendelea
Mamlaka za Venezuela zimeeleza kuwa ukiacha mji mkuu Caracas maeneo mengine ya majimbo ya Miranda, Aragua na La Guaira nayo yameshambuliwa na helikopta za wamarekani
Kufuatia taarifa za Rais Maduro kuchukuliwa, Makamu wa Rais wa Venezuela Delcy Rodrigaz ameripotiwa na vyombo vya habari nchini humo kuwa Serikali ya Venezuela bado haifahamu chochote juu ya alipo Rais wa Nchi hiyo na kutaka kuhakikishiwa usalama wake na sheria za kimataifa kuzingatiwa.
Waziri wa Ulinzi wa Venezuela, ambaye awali iliripotiwa kuwa ameuwawa baada ya makazi yake kushambuliwa, ameonekana katika video iliyosambaa kuwataka wananchi wa Venezuela kuwa watulivu na kwamba mamlaka za nchi hiyo zimeshachukua hatua za kukabiliana na uvamizi huo aliouita wa kibeberu.
Unaweza kutufuatilia kupitia;
TWITTER: / thechanzo
INSTAGRAM: / thechanzo
FACEBOOK: / thechanzo
TIKTOK: https://www.tiktok.com/@thechanzo?is_...
Au tembelea tovuti yetu: https://www.thechanzo.com
Je, una habari? wasiliana nasi kupitia Telegram/WhatsApp +255 753 815 105
The Chanzo 2025 © All Rights Reserved.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: