WAZIRI WA ULINZI DKT. STERGOMENA TAX Awaaga Watumishi wa Wizara na Kuwapa Ujumba huu...
Автор: Ulinzi Channel
Загружено: 2025-10-18
Просмотров: 3673
Описание:
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax tarehe 16 Oktoba, 2025 amefanya mazungumzo na Wafanyakazi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ambapo pamoja na mambo mengine ametumia wasaa huo kuwaaga wafanyakazi baada ya kumaliza muda wake wa Utumishi Kikatiba katika wizara ya Ulinzi kufuatia Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025 nchini kote.
Waziri Stergomena amezungumza na kuwaaga Wafanyakazi hao katika Ukumbi wa Mabele wa Jijini Dodoma na kuwashukuru wafanyakazi wa Wizara kwa ushirikiano wao waliomuonyesha na kumpatia katika kipindi chote alichohudumu kama Waziri wa Ulinzi.
Amewashukuru wafanyakazi hao kwa mshikamano waliouonyesha, kujituma, uadilifu na moyo wa kizalendo na Weledi wa kila mmoja kwa nafasi yake waliomuonyesha kwa muda wote wa utumishi wake.
“Waswahili husema Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu kauli hii imejidhililisha wazi katika Utendaji wetu”, akaongeza, “hata ukiwa na uwezo mkubwa kiasi gani ni vigumu kufanikisha mambo peke yako hususani mambo makubwa, hata ukijigamba kuwa umefanikisha peke yako uhalisia utaonyesha kuwa ipo michango kwa waliokusaidia au ulioshirikiana nao hivyo basi natambua mchango wa kila mmoja wenu” alisisitiza Waziri Stergomena Tax.
Waziri wa Ulinzi na JKT, Dkt Stergomena, akachukua fursa hiyo pia kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumteua kuhudumu katika nafasi hiyo adhimu kama Wazari wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa mara mbili Septemba 2021 hadi Oktoba 2022 na mara ya pili Agosti 2023 hadi sasa Oktoba 2025 ambapo amehudumu katika Wizara ya Ulinzi na JKT kwa jumla miaka mitatu.
Awali akimkaribisha Waziri wa Ulinzi ili aongee na wafanyakazi, Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na JKT Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe alimpongeza Waziri Stergomena kwa uongozi wake mahiri na kusema anajivunia kwa kuwa amekuwa Katibu Mkuu wa kwanza kuongozwa na Waziri wa Ulinzi na JKT wa kwanza Mwanamke tangu nchi yetu ipate Uhuru.
Hafla ya Waziri wa Ulinzi na JKT kuongea na kuwaaga Wafanyakazi ilihudhuriwa pia na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Ulinzi, Makamishna wa Wizara, Maafisa Jenerali, Maafisa wakuu na wadogo na askari pamoja na watumishi wa umma wa Wizara ya Ulinzi na JKT.
#wizarayaulinzi #jwtz #jkt #DktStergomenaTax #WaziriwaUlinzi
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: