MUBASAHARA (LIVE) KUPITIA TBC
Автор: MKOA WA SONGWE
Загружено: 2026-03-11
Просмотров: 161
Описание:
Kamanda wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Itaka, Kanali Gelvas Chitola, amezungumza mubashara (live) kupitia chombo cha Habari cha Taifa TBC, akiwa katika eneo la Kimondo, Kata ya Ndolezi, Wilayani Mbozi.
Akizungumza katika mahojiano hayo, Kanali Chitola ameeleza kuhusu mafunzo ya uzalendo na uzalishaji yanayotolewa katika Kikosi cha JKT Itaka, akibainisha kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwajengea vijana nidhamu, uzalendo kwa Taifa pamoja na kuwapa ujuzi wa uzalishaji mali ili waweze kujitegemea.
Amesema kupitia mafunzo hayo, vijana hupata fursa ya kujifunza stadi mbalimbali za kazi pamoja na kushiriki katika shughuli za uzalishaji zinazochangia maendeleo ya Taifa na jamii kwa ujumla.
Aidha, amesisitiza kuwa JKT itaendelea kushirikiana na Serikali na wadau mbalimbali kuhakikisha vijana wengi zaidi wanapata mafunzo hayo muhimu kwa ajili ya kujenga Taifa lenye vijana wenye maadili, uzalendo na uwezo wa kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: