ycliper

Популярное

Музыка Кино и Анимация Автомобили Животные Спорт Путешествия Игры Юмор

Интересные видео

2025 Сериалы Трейлеры Новости Как сделать Видеоуроки Diy своими руками

Топ запросов

смотреть а4 schoolboy runaway турецкий сериал смотреть мультфильмы эдисон
Скачать

RC MALIMA AKAGUA RELI YA SGR MORO – KILOSA.

Автор: RS MOROGORO

Загружено: 2024-07-05

Просмотров: 242

Описание: RC MALIMA AKAGUA RELI YA SGR MORO – KILOSA.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha kutoka Morogoro hadi Kilosa kwa lengo la kuangalia hatua ya ujenzi iliyofikiwa pamoja na usalama wa treni hiyo inayotarajia kuanza safari zake katikati ya mwezi Julai 25, mwaka huu.

Mhe. Malima amefanya ziara hiyo Julai 4, 2024 akiambatana na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ikiwa ni maandalizi ya utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan la kutaka treni hiyo kuanza safari zake kwa kipande cha Morogoro – Dodoma ifikapo Julai 25, Mwaka huu.

Katika ziara hiyo, Mkuu huyo wa Mkoa amesema ameridhishwa na utendaji kazi unaoendelea wa kukamilisha ujenzi wa miundo mbinu ambayo ilikuwa haijakamilika ikiwemo ujenzi wa uzio (Fence) kwa ajili ya kuzuia wanyama pori kama tembo pamoja na mifugo huku akiagiza kazi hiyo ikamilike ifikapo tarehe 15 - 18 Julai.

“…sisi watu wa Morogoro tulipokea salamu, ya kwamba kuanzia tarehe 25 mwaka huu zitaanza safari za abiria kwenda Dodoma lakini kwa muda sasa, zaidi ya mwezi tuliweka angalizo kwa eneo hili…” amesema Mhe. Malima

Akikagua kituo cha treni cha Kilosa Mkuu huyo wa Mkoa amesema Kituo hicho cha treni cha Kilosa ni cha kimkakati kwa kuwa kitasaidia kukuza sekta ya Utalii Mkoani humo kwani amesema wageni wengi watakaotumia usafiri wa SGR wataweza kushuka Kilosa na kisha kutembelea Vivutio vilivyopo Mkoani humo vikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Nyerere, Mbuga ya Wanyama ya Mikumi, Hifadhi ya Milima ya Udzungwa, na vivutio vingine vingi vilivyopo eneo hilo.

Katika hatua nyingine Mhe. Adam Kighoma Malima amekemea vikali tabia ya baadhi ya wananchi wanaojihusisha na wizi wa miundombinu ya Reli hiyo zikiwemo Nyaya za shaba huku akiwaonya kuwa watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria na mpaka sasa amesema tayari kuna baadhi ya watu wameshatiwa mbaroni wakihusishwa na wizi wa vifaa vya mradi huo.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kilosa Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amesema Kituo cha treni cha mwendokasi cha Kilosa kitafungua milango ya kiuchumi hususan katika sekta ya Utalii, Kilimo na Mifugo ambapo kumewekwa mkakati wa kushawishi watalii kutoka ndani na nje ya nchi kuanza kutembelea Vivutio na uwekezaji uliomo ndani ya Kilosa kupitia Reli ya SGR.

Hata hivyo, Mhe. Kabudi amebainisha kuwa Wilaya ya Kilosa ina utajiri wa kilimo cha mazao mbalimbali likiwemo zao la Vitunguu na mpunga hivyo kutokana na urahisi wa usafirishaji wa mazao hayo kutachochea uzalishaji wenye tija na kujenga Uchumi wa Wilaya, Mkoa na Taifa kwa jumla.

Naye, Mkurugenzi wa Miundombinu wa Shirika la reli Tanzania Mhandisi Machibya Shiwa amesema zoezi la kuweka uzio limefikia 95% huku maeneo ya ushoroba wa Ngerengere na ushoroba uliopo katikati ya Kimambila na kimamba ni maeneo yanayojengwa uzio maalum wa kudhibiti wanyama wakiwemo tembo wanaotoka mbuga ya Mikumi.

Mwisho

Не удается загрузить Youtube-плеер. Проверьте блокировку Youtube в вашей сети.
Повторяем попытку...
RC MALIMA AKAGUA RELI YA SGR MORO – KILOSA.

Поделиться в:

Доступные форматы для скачивания:

Скачать видео

  • Информация по загрузке:

Скачать аудио

Похожие видео

#Kaziiendelee KILOSA DARAJA REFU MTO MKONDOA, UTANDIKAJI RELI NA UTOFAUTI WAKE

#Kaziiendelee KILOSA DARAJA REFU MTO MKONDOA, UTANDIKAJI RELI NA UTOFAUTI WAKE "MAHANDAKI YOTE 100%"

Mradi wa Handeni, Korogwe, Muheza na Pangani umefikia asilimia 74 ya utekelezaji  wake.

Mradi wa Handeni, Korogwe, Muheza na Pangani umefikia asilimia 74 ya utekelezaji wake.

#TRENI YA DELUXE IVYOSIMAMA PEMBENI YA MTO MKONDOA NA DIAMOND KUSHUHUDIA HANDAKI LA TRENI YA SGR

#TRENI YA DELUXE IVYOSIMAMA PEMBENI YA MTO MKONDOA NA DIAMOND KUSHUHUDIA HANDAKI LA TRENI YA SGR

Россия прорвала блокаду. Новый Ил-114-300 покоряет Индию

Россия прорвала блокаду. Новый Ил-114-300 покоряет Индию

Dkt. Kijaji aitaka TANAPA kutafuta mkandarasi mpya

Dkt. Kijaji aitaka TANAPA kutafuta mkandarasi mpya

MICHE MILIONI 30 KUPANDWA MOROGORO

MICHE MILIONI 30 KUPANDWA MOROGORO

VITASA | Tukio zima la Kibwana Shomari kufanyiwa tambiko na kuagwa Morogoro

VITASA | Tukio zima la Kibwana Shomari kufanyiwa tambiko na kuagwa Morogoro

RC KASKAZINI PEMBA AWAKARIBISHA WANANCHI WOTE KATIKA UFUNGUZI WA BARABARA YA CHAKE -  WETE

RC KASKAZINI PEMBA AWAKARIBISHA WANANCHI WOTE KATIKA UFUNGUZI WA BARABARA YA CHAKE - WETE

Почки скажут вам: всего 1 стакан перед сном и ночные походы в туалет исчезнут | ПАМЯТЬ И МОЗГ

Почки скажут вам: всего 1 стакан перед сном и ночные походы в туалет исчезнут | ПАМЯТЬ И МОЗГ

РЫСЬ В ДЕЛЕ... Рысь против волка, койота, змеи, оленя!

РЫСЬ В ДЕЛЕ... Рысь против волка, койота, змеи, оленя!

История Византии за 13 минут

История Византии за 13 минут

⚡ЭТО СКРЫВАЛИ 20 ЛЕТ. Архивные КАДРЫ Путина ШОКИРОВАЛИ признанием Ичкерии. Все что нужно знать об РФ

⚡ЭТО СКРЫВАЛИ 20 ЛЕТ. Архивные КАДРЫ Путина ШОКИРОВАЛИ признанием Ичкерии. Все что нужно знать об РФ

RC MALIMA ATEMA CHECHE MGOGORO WA BARABARA, ATOA SIKU 7 KUMALIZIKA.

RC MALIMA ATEMA CHECHE MGOGORO WA BARABARA, ATOA SIKU 7 KUMALIZIKA.

Немцы не знали, что поймали офицера НКВД, который был лучшим инструктором из спецшколы

Немцы не знали, что поймали офицера НКВД, который был лучшим инструктором из спецшколы

CHUO CHA RELI  TIRTEC NA UKUAJI WA SEKTA YA RELI NCHINI I MAANDALIZI YA MAHAFALI YA NNE-TABORA

CHUO CHA RELI TIRTEC NA UKUAJI WA SEKTA YA RELI NCHINI I MAANDALIZI YA MAHAFALI YA NNE-TABORA

RC Malima aiagiza TANROADS kuongeza alama za barabara Iyovi.

RC Malima aiagiza TANROADS kuongeza alama za barabara Iyovi.

MIAKA MITANO YA RAIS DKT. SAMIA: MAPINDUZI MAKUBWA YASHUHUDIWA SEKTA YA AFYA – RC MALIMA.

MIAKA MITANO YA RAIS DKT. SAMIA: MAPINDUZI MAKUBWA YASHUHUDIWA SEKTA YA AFYA – RC MALIMA.

Образование Русского государства - на карте

Образование Русского государства - на карте

Что произошло с лидером Ливии Каддафи в последние часы перед его убийством?

Что произошло с лидером Ливии Каддафи в последние часы перед его убийством?

WETANGULA REGRETS IMPEACHING GACHAGUA AFTER THIS NIS REPORT!

WETANGULA REGRETS IMPEACHING GACHAGUA AFTER THIS NIS REPORT!

© 2025 ycliper. Все права защищены.

  • Контакты
  • О нас
  • Политика конфиденциальности

Контакты для правообладателей: [email protected]