Tazama meli kubwa Mv Mwanza ‘Hapa Kazi Tu’ ikianza majaribio mbele ya Waziri
Автор: Mwananchi Digital
Загружено: 2024-03-27
Просмотров: 3050
Описание:
Cheza sasa kupitia https://shorturl.at/jqzU6 na ushinde
Meli ya Mv Mwanza ‘Hapa Kazi Tu’ inayojengwa katika bandari ya Mwanza imeanza kufanyiwa majaribio huku ujenzi wake ukifikia asilimia 93.
Ujenzi wa meli hiyo inayogharimu zaidi ya Sh125 bilioni ulianza Septemba 2019 na inatarajiwa kuanza kutoa huduma ya usafirishaji wa abiria na mizigo Julai, 2024.
Meli hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 1,200, tani 400 za mizigo, magari madogo 20 na makubwa matatu; itakapokamilika inatarajiwa kutoa huduma ndani ya Ziwa Victoria katika nchi ya Tanzania, Kenya na Uganda.
Akizungumza baada ya kushuhudia majaribio ya meli hiyo, Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema majaribio ya meli hiyo yatafanyika kwa awamu tatu kwa kuzingatia viwango vya kimataifa (ISO) kabla ya kuanza kutoa huduma.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: