Esther MATIKO Afafanua MIRADI MIKUBWA Inayotekelezwa na Dkt. Samia Mkoa wa MARA!
Автор: MANONGA TV
Загружено: 2026-01-30
Просмотров: 55
Описание:
MBUNGE wa Jimbo la Tarime Mjini (CCM), Mhe. Esther Nicholas Matiko 'Msubhati' ameeleza na kupongeza miradi mingi ya maendeleo inayoendelea kufanyika katika Jimbo la Tarime Mjini na Mkoa wa Mara kwa ujumla, huku akiwahakikishia wananchi wa Tarime Mjini kupata huduma bora za mahitaji muhimu ya kijamii.
Mhe. Matiko ameweka bayana juu y miradi hiyo mapema leo Bungeni, wakati akiwasilisha mchango wake kwa hotuba ya Rais Dkt. Samia, aliyoitoa wakati wa uzinduzi wa Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Novemba mwaka 2025.
Miongoni mwa miradi mikubwa aliyoiainisha Mhe. Matiko ni pamoja na mradi mkubwa wa Maji, unaounganisha wilaya za Tarime na Rorya, pamoja na uwepo wa viwanja vikubwa vya ndege, kikiwemo cha Wilaya ya Serengeti
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: