VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA MKOANI GEITA VYAHIMIZA KULINDA AMANI
Автор: BM MULTIMEDIA Digital Production
Загружено: 2025-10-27
Просмотров: 882
Описание:
VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA MKOANI GEITA VYAHIMIZA KULINDA AMANI
Geita – Vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Geita vimewashukuru wachungaji, viongozi wa dini na viongozi mbalimbali kwa maombi yao yanayochangia kuwepo kwa amani na utulivu nchini.
Akizungumza katika kongamano la maombi lililofanyika katika viwanja vya EPZA mjini Geita, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Amon Challe Mimata, amesema maombi ya viongozi wa dini yamekuwa na mchango mkubwa katika kuwezesha vyombo vya ulinzi kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kwa amani.
“Tunawashukuru sana viongozi wa dini kwa maombi yenu. Maombi haya yanatupa nguvu na kutuwezesha kufanya kazi katika mazingira ya utulivu. Tunaomba muendelee kuombea nchi yetu na kuilinda amani kuanzia ngazi ya familia,” alisema ACP Mimata.
Amesisitiza umuhimu wa kila mwananchi kushiriki katika kulinda tunu ya amani ambayo Tanzania imeibarikiwa kuwa nayo kwa muda mrefu, akieleza kuwa jukumu hilo si la vyombo vya ulinzi pekee bali ni la kila mmoja.
“Amani inaanzia nyumbani. Tuishi kwa upendo, tufanye upatanisho na majirani zetu, tuwe watu wa maelewano. Huo ndio msingi wa amani ya kudumu,” aliongeza.
ACP Mimata pia alibainisha kuwa vyombo vya ulinzi mkoani Geita vimejipanga kuhakikisha amani inaimarishwa kabla, wakati na baada ya Uchaguzi, kwa kushirikiana na wananchi na taasisi mbalimbali.
Kongamano hilo la maombi lilihudhuriwa na viongozi wa serikali, vyombo vya ulinzi na usalama, viongozi wa dini kutoka madhehebu mbalimbali, pamoja na wawakilishi wa vyama vya siasa, wote wakijumuika kwa lengo la kuombea amani na umoja wa taifa.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: