ycliper

Популярное

Музыка Кино и Анимация Автомобили Животные Спорт Путешествия Игры Юмор

Интересные видео

2025 Сериалы Трейлеры Новости Как сделать Видеоуроки Diy своими руками

Топ запросов

смотреть а4 schoolboy runaway турецкий сериал смотреть мультфильмы эдисон
Скачать

UZALISHAJI MAGARI YA UMEME UGANDA, MCHONGO TANZANIA

Автор: Mwananchi Digital

Загружено: 2024-08-16

Просмотров: 2581

Описание: Wakati Uganda ikifungua kiwanda kutengeneza magari ya umeme, wadau wameeleza kuwa hatua hiyo ni fursa kwa nchi jirani ikiwemo Tanzania kupunguza matumizi ya fedha za kigeni zinazotumika kuagiza mafuta kila mara.

Kiwanda hicho kwa kwanza Afrika kuzalisha magari ya umeme, Kiira Motors Coorporation (KMC), kinatarajiwa kuzalisha magari 5,000 kwa mwaka yatakayohusisha magari mabasi madogo ya abiria na yale ya masafa marefu.

Takwimu zinaonyesha Tanzania kwa mwaka Tanzania hutumia wastani wa lita bilioni 4 za mafuta ambazo gharama yake hubadilika mara kwa mara kutokana na kupanda kwa thamani ya dola na gharama za usafirishaji.

Katibu wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa), Joseph Priscus amesema kuanzishwa kwa kiwanda hicho ni hatua kubwa katika biashara ya usafirishaji na utekelezaji wake utakuwa na manufaa pia kwa nchi.

Akizungumza leo Agosti 16, 2024 wakati wa ufunguzi wa kiwanda hicho sambamba na maonesho ya vyombo vya moto vinavyotumia umeme, Priscus amesema endapo teknolojia ya magari ya umeme itashika kasi, itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama za uendeshaji na nchi itapata mapato yatokanayo na mauzo ya umeme.

Amesema Tanzania inatumia kiasi kikubwa cha fedha za kigeni kuagiza mafuta kutoka nje ya nchi hivyo endapo magari ya umeme yataanza kutumika, fedha hizo zitabaki nchini kwa ajili ya matumizi mengine.

Amesema kwa muda mrefu kumekuwa na mabadiliko katika bei za mafuta, hali inayosababisha kuyumbisha biashara ya usafirishaji, hivyo teknolojia ya gesi na umeme ni mkombozi.

“Hiki kiwanda kipo Uganda lakini sisi kama nchi jirani naona tunaweza kuitumia fursa hii na kupata manufaa. Kama nchi tunatumia fedha nyingi kuagiza mafuta lakini tukiwa na magari haya, hatuna sababu ya kutumia fedha hizo kwa sababu umeme tunao.

“Tunaona hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha tunakuwa na umeme wa uhakika, ikiwemo ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere, hivyo nishati ya umeme tunayo ya kutosha kwa ajili ya magari haya,” amesema Priscus na kuongeza:

“Mbali na faida ambazo Serikali itapata kupitia mauzo ya umeme, kwa upande wetu wafanyabiashara magari haya yatapunguza gharama za uendeshaji kwa kuwa teknolojia hii haina matumizi makubwa ya vilainishi wala matengenezo ya mara kwa mara.”

Mkurugenzi Mkuu wa Kiira Motors, Paul Musasizi amesema Serikali ya Uganda imetumia dola 85 milioni (Sh230 bilioni) kufanya uwekezaji huo unaoenda kuifanya kuwa nchi ya kwanza Afrika Mashariki na kati kuwa kiwanda cha kutengeneza magari ya umeme.

Amesema tayari kiwanda hicho kimeshazalisha magari 40 ambayo yameanza kutoa huduma ya kubeba abiria katika miji ya Entebe, Jinja na Kampala.

Amesema mpango wa kuwa na kiwanda hicho ulianza 2007 kwa kupeleka wataalamu nje kujifunza tekinolojia hiyo na hatimaye waliweza kutengeneza magari hayo nchini Uganda kupitia kiwanda kidogo, kabla ya kuanzisha kiwanda kikubwa ambacho kitazinduliwa Oktoba mwaka huu.

Не удается загрузить Youtube-плеер. Проверьте блокировку Youtube в вашей сети.
Повторяем попытку...
UZALISHAJI MAGARI  YA UMEME UGANDA, MCHONGO TANZANIA

Поделиться в:

Доступные форматы для скачивания:

Скачать видео

  • Информация по загрузке:

Скачать аудио

Похожие видео

VIJANA TANGA WAUNDA BAJAJI ZINAZOTUMIA MFUMO WA UMEME,

VIJANA TANGA WAUNDA BAJAJI ZINAZOTUMIA MFUMO WA UMEME, "UMEME WA 2000 TU KWA KILOMITA 100"

Жёсткий ответ России из Азербайджана! Баку выйдет из СНГ?

Жёсткий ответ России из Азербайджана! Баку выйдет из СНГ?

MAGARI YASIYOTUMIA MAFUTA YAGUNDULIWA TANZANIA, YANATUMIA UMEME WA JUA, YANATEMBEA HADI KM 120..

MAGARI YASIYOTUMIA MAFUTA YAGUNDULIWA TANZANIA, YANATUMIA UMEME WA JUA, YANATEMBEA HADI KM 120..

TAZAMA JWTZ YAUNDA MAGARI AINA YA NYUMBU, VIFARU, ZIMAMOTO, MITAMBO, VIPULI, KAMANDA AFUNGUKA

TAZAMA JWTZ YAUNDA MAGARI AINA YA NYUMBU, VIFARU, ZIMAMOTO, MITAMBO, VIPULI, KAMANDA AFUNGUKA

SIKIA JINSI WAMALAWI WANAVYOIZUNGUMZIA NCHI YA TANZANIA

SIKIA JINSI WAMALAWI WANAVYOIZUNGUMZIA NCHI YA TANZANIA

Shirika la TATC NYUMBU Kibaha  lakabidhiwa Mashine za kisasa za Bolts and Nuts

Shirika la TATC NYUMBU Kibaha lakabidhiwa Mashine za kisasa za Bolts and Nuts

NDEGE KUBWA KUANZA KUTUA TANGA BAADA YA MABORESHO MAKUBWA YA UWANJA, N/WAZIRI AELEZA

NDEGE KUBWA KUANZA KUTUA TANGA BAADA YA MABORESHO MAKUBWA YA UWANJA, N/WAZIRI AELEZA

EXCLUSIVE: KIWANDA CHA MAGARI YA VOLKSWAGEN RWANDA, WANATUMIA MAGARI YA UMEME MTAANI

EXCLUSIVE: KIWANDA CHA MAGARI YA VOLKSWAGEN RWANDA, WANATUMIA MAGARI YA UMEME MTAANI

BAJAJI ZA UMEME DSM, UNA CHAJI, INAOKOA ELFU 40

BAJAJI ZA UMEME DSM, UNA CHAJI, INAOKOA ELFU 40

KIINGEREZA CHA MBUNGE WA UKONGA KILIVYOPEPERUKA WENGINE WAKIWASHA NAFASI NYETI IPU

KIINGEREZA CHA MBUNGE WA UKONGA KILIVYOPEPERUKA WENGINE WAKIWASHA NAFASI NYETI IPU

Prof Jay awapagawisha Wanamorogoro mbele ya JPM

Prof Jay awapagawisha Wanamorogoro mbele ya JPM

KIWANDA CHA MIFUKO YA KARATASI MTWARA KUTOA AJIRA.

KIWANDA CHA MIFUKO YA KARATASI MTWARA KUTOA AJIRA.

Почему Польша купила тысячу корейских танков вместо Абрамсов и Леопардов?

Почему Польша купила тысячу корейских танков вместо Абрамсов и Леопардов?

Хиросима: День, когда упало небо | Многоязычный документальный фильм

Хиросима: День, когда упало небо | Многоязычный документальный фильм

Ukichaji gari hili la umeme nyumbani kwa umeme wa elfu 20 unatembea kwa zaidi ya kilometa 300

Ukichaji gari hili la umeme nyumbani kwa umeme wa elfu 20 unatembea kwa zaidi ya kilometa 300

NAPE NNAUYE -

NAPE NNAUYE - "UTU TUUONE VYOMBO vya DOLA - TUKIMUNG'UNYA MANENO CCM ITAONDOKA JAMANI"....

#TBC1 WEKEZA TANZANIA: TAZAMA UWEKEZAJI WA MJI WA VIWANDA WA KIGAMBONI - DSM

#TBC1 WEKEZA TANZANIA: TAZAMA UWEKEZAJI WA MJI WA VIWANDA WA KIGAMBONI - DSM

То, что Китай строит прямо сейчас, лишит вас дара речи

То, что Китай строит прямо сейчас, лишит вас дара речи

С какой скоростью движется Земля во Вселенной? [Космос 2024]

С какой скоростью движется Земля во Вселенной? [Космос 2024]

Двигатели Tesla Илона Маска против электромобилей Kiira из Уганды | что лучше?

Двигатели Tesla Илона Маска против электромобилей Kiira из Уганды | что лучше?

© 2025 ycliper. Все права защищены.

  • Контакты
  • О нас
  • Политика конфиденциальности

Контакты для правообладателей: [email protected]