HIGHLIGHTS: SUDAN 0-5 TANZANIA (CECAFA U17 AFCON QUALIFIER)
Автор: Azam TV
Загружено: 2018-08-16
Просмотров: 429823
Описание:
Tanzania imeendelea kufanya vizuri katika michuano ya vijana ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kwa vijana chini ya miaka 17 ambayo inatumika kuwania kufuzu Kombe la Afrika (AFCON) baada ya leo jioni kuichapa Sudan mabao 5-0.
Wakiwa chini ya Kocha Oscar Milambo, vijana wa Tanzania maarufu kama Serengeti Boys walicheza soka safi na la kuvutia na kufanikiwa kupata bao la kwanza dakika ya kumi tu ya mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Bao hilo la kwanza la Tanzania lilitokana na mchezaji wao Omer Yousif kujifunga akiwa katika harakati za kuokoa. Tanzania ilipata bao la pili katika dakika ya 45 mfungaji akiwa ni Kelvin John.
Kelvin aliifungia Tanzania bao la tatu dakika ya 60 na kuanzia hapo wenyeji walitawala mchezo huku wachezaji wa Sudan wakionekana kuchoka hivyo kushindwa kuumudu mchezo huo.
Dakika ya 72, Agiri Ngoda aliifungia Tanzania bao la nne na dakika saba baadaye alifunga bao la tano na kuifanya Serengeti Boys kutoka uwanjani hapo na ushindi wa mabao 5-0.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: