MBUNGE KISHOA AZINDUA KLINIKI TEMBEZI YA MIKOPO YA ASILIMIA 10 MKALAMA.
Автор: CLOUDS HABARI
Загружено: 2026-03-16
Просмотров: 5
Описание:
MBUNGE KISHOA AZINDUA KLINIKI TEMBEZI YA MIKOPO YA ASILIMIA 10 MKALAMA.
Mbunge wa Jimbo la Iramba Mashariki, Jesca Kishoa, amewahimiza wananchi kutumia vizuri mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na serikali ili kuboresha mitaji ya biashara na miradi ya maendeleo.
Kishoa ameyasema hayo Machi 16, 2026 katika Kata ya Nkalakala Wilayani Mkalama wakati wa uzinduzi wa Kliniki Tembezi ya Mikopo ya Asilimia 10 inayotolewa kwa Vijana, wanawake na watu wenye ulemavu wa Wilaya ya Mkalama.
“Mikopo ya asilimia 10 ni nguzo muhimu inayosaidia kuboresha mitaji ya wananchi wenye pato la chini ili waweze kuendeleza miradi na biashara zao,” amesema Kishoa.
Amesema pia kuwa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 inalenga kuifikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati kwenda juu kupitia maendeleo ya viwanda, teknolojia na ubunifu.
“Wananchi mnapaswa kuwekeza katika nyanja mbalimbali za kiuchumi ili kufikia adhima ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 ya kuwa na uchumi wa juu,” amesema.
Aidha, amewahimiza wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kutumia vyema fursa ya mikopo hiyo nafuu ili kuimarisha shughuli zao za kiuchumi.
Kishoa pia amesisitiza umuhimu wa nidhamu katika matumizi ya mikopo hiyo kwa kuhakikisha fedha zinazotolewa zinatumika kwa malengo ya vikundi husika badala ya kugawanywa kwa matumizi mengine.
“Mnahimizwa kuwa na nidhamu ya fedha za mikopo mnayopatiwa na serikali kwa kuhakikisha mnazitumia kwa malengo mahsusi ya kikundi chenu na si kugawana,” amesema.
@@officialrobertnho
#Cloudsdigtalupdates
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: