AJALI YASABABISHA UTEKELEZWAJI WA HARAKA WA UJENZI WA BARABARA YA MCHEPUKO MBEYA
Автор: KUSAGA TV
Загружено: 2025-06-11
Просмотров: 2417
Описание:
Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan la kutengeneza barabara ya mchepuko katika eneo la Iwambi jijini Mbeya ili kupunguza madhara yatokanayo na ajali za barabarani limeanza kutekelezwa na wakala wa barabara Tanzania TANROADS mkoa wa Mbeya.
Akizungumza katika eneo unakofanyika utengezaji wa barabara hiyo mkuu wa wilaya ya Mbeya Beno Malisa amesema tayari agizo hilo limeanza kufanyiwa kazi na wakala wa barabara Tanzania TANROADS mkoa wa Mbeya.
Kuhusu agizo la kulipwa fidia kwa wananchi mkuu wa wilaya anasemaje.
Mhandisi Masige Matari ni meneja wakala wa barabara Tanzania TANROADS mkoa wa Mbeya yeye anaeleza namna anavyotekeleza agizo la rais.
Juni saba mwaka huu katika eneo la Iwambi jijini Mbeya jumla ya watu 28 walifariki dunia na wengine tisa kujeruhiwa kufuatia ajali iliyohusisha magari matatu lori aina ya Scania lenye namba za usajili T 830 EDP lenye tela namba T 148 CTD, Coaster aina ya Mitsubishi Rosa lenye namba za usajili T 257 DVP na gari lingine aina ya Toyota Lite Hiace lenye namba za usajili T 185 DMF baada ya wa dereva wa lori aina ya Scania lenye namba za usajili T 830 EDP lenye tela namba T 148 CTD kuendesha gari kwa mwendokasi na kushindwa kulimudu gari lake na hivyo kuyagonga magari mengine mawili.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: