WAFUKUA KABURI SINGIDA SITA WASHIKWA
Автор: Chamber Talkshow
Загружено: 2023-03-28
Просмотров: 411
Описание:
Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida limefanikiwa kukamata watuhumiwa 6 wanaojihusisha na matukio ya mauaji na ufukuaji wa makaburi yanayotokana na Imani za kishirikina katika Wilaya ya manyoni Mkoa wa Singida.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida Stella Mutabihiriwa Amesema katika mahojiano yaliyofanywa na Jeshi la Polisi watuhumiwa hao wamekiri kuhusika na ,tukio la mauaji lililotokea tarehe 3/3/2023 eneo la relini Manyoni ambapo MTU mmoja mwanamke ambaye kina lake halikufahamika mwenye umri wa miaka 40-45 alikutwa amefariki huku kifi chake kikihusishwa na treni.
Aidha STELLA Amesema baadhi ya Sehemu ya viungo vya marehemu hiyo vilikuwa pembeni mwa njia ya TREN na kiwiliwili kikibaki katikati ya njia ya TREN huku viungo vya Sehemu za Siri vikiwa vimenyofolewa kitendo ambacho wamekiri kuhusika na tukio Hilo na kuelezea kuwa walikata Sehemu za Siri,nywele,kucha na ulimi Kwa lengo la kutengeneza dawa Ili kupata wateja wanaoitaji utajiri.
Vile vile watuhumiwa hao wamekiri kujihusisha na vitendo vya kufukua makaburi wilayani Manyoni sambamba na kuua watu Kwa lengo la kupata viungo vya Sehemu za Siri vya binadamu Kwa ajili ya kutengeneza dawa ya kupata utajiri.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida linatoa wito Kwa wananchi hasa Wilaya ya Manyoni ambako vitendo hivi vya kishirikina vimeshamiri kuachana na Imani potofu za kishirikina vinavyopelekea watu kutafuta utajiri katika njia zisizo halali na kuwataka wananchi kufanya Kazi Kwa Bidii.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: