Kaya 14 zakosa makazi Moshi baada ya nyumba zao kuzingirwa na mafuriko
Автор: Mwananchi Digital
Загружено: 2026-03-04
Просмотров: 335
Описание:
Moshi.Kaya 14 zenye watu zaidi ya 39 katika mtaa wa Viwanda, kata ya Njoro, Manispaa ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro hazina mahali pakuishi baada ya nyumba zao kuzingirwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha kwa zaidi ya saa sita usiku wa kuamkia Machi 2, mwaka huu.
Mbali na kukosa mahali pakuishi, familia hizo zinakabiliwa na uhaba wa chakula baada ya vyakula vyao kuharibiwa na maji ya mafuriko, ambapo wameiomba serikali kuwapa msaada wa dharura ili kuzinusuru kaya hizo.
Wakizungumza na Mwananchi leo Machi 3, 2026 baadhi ya waathirika wa mafuriko hayo, wameiomba serikali kuwapatia msaada wa vyakula na malazi kwakuwa vitu walivyokuwa navyo ndani ikiwemo magodoro, vitanda, vifaa vya watoto wa shule pamoja na vitu vingine viliathiriwa na mafuriko hayo.
Naye, mjumbe wa serikali ya mtaa huo, William Kavishe amesema kaya nyingi za mtaa huo zimeathiriwa na mafuriko hayo na kwamba watu 39 hawana mahali pakuishi baada ya nyumba zao kuzingirwa na mafuriko hayo.
Akizungumza Mkuu wa Wilaya hiyo, Godfrey Mnzava amesema baadhi ya wananachi walioathiriwa na mafuriko hayo ni wale ambao wapo mabondeni na ndani ya mita 60 ya mto Njoro na kwamba kaya 14 zenye watu 39 ndio zimeathiriwa na mafuriko hayo.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: