Huzuni!!! Mwili wa Neech Msuya wazikwa , mtoto ashindwa kujizuia aangua kilio upyaa
Автор: Mwananchi Digital
Загружено: 2023-08-06
Просмотров: 12640
Описание:
Mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa maafa katika benki ya ABSA, Neech Msuya umezikwa leo nyumbani kwao katika kijiji cha Msangeni, kata ya Msangeni Ugweno, Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro.
Neech Msuya pamoja na dada zake watatu, Sia,Diana na Norah, walifariki dunia Agosti 3, mwaka huu, kwa ajali ya gari iliyotokea katika kijiji cha Mapatano, Kata ya Mbwewe mkoani Pwani, wakati wakielekea Ugweno kwenye msiba wa mtoto wa baba yao mdogo.
Katika ibada hiyo ambayo iligubikwa na vilio na simanzi, ilihudhuriwa na mamia ya waombolezaji wakiwemo viongozi wa dini, ambapo kila aliyesimama ameisihi familia kumtazama Mungu kama mfariji wao mkuu kwa kuwa yeye ndiye kila kitu.
Ibada hiyo ya mazishi iliongozwa na Mchungaji kiongozi wa usharika wa Msangeni Dayosisi ya Mwanga ya Kanisa la Kiinjili la Kikutheri Tanzania (KKKT) Charles Tenga huku mahubiri yakitolewa na mchungaji wa Ndanda Anituja Msuya.
Katika mahubiri yake yake Mchungaji Msuya amesema kifo ni mpango wa Mungu na kuwataka wazazi kusimama kumtazama
Mwakilishi wa benki ya ABSA Patrick Foya, amesema habari za kifo cha Neech zimewaumiza na kwamba hawana maneno mazuri ya kuweza kuwafariji wazazi ila cha msingi ni kuwakabidhi katika mikono ya Mungu.
Baada ya Neech kuzikwa leo Kijiji cha Msangeni Ugweno, familia itanza safari kesho Jumatatu kuelekea Dar es Salaam kwa ajili ya mazishi ya dada zake ambayo yatafanyika jumanne Agosti 8, mwaka huu.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: