Sheria kama Ahadi ya Mungu kwa Ajili Yetu: Yesu ni Utimilifu wa Sheria | Lesson 8 || 20 August 2025
Автор: Maisha Kamili
Загружено: 2025-08-21
Просмотров: 217
Описание:
Muhtasari:
Paulo anasisitiza kuwa wokovu haupatikani kwa kuzishika Amri Kumi (Rum. 3:20-24), bali kupitia neema ya Kristo. Hata hivyo, amri hufanya kazi ya kutufunulia udhaifu wetu na hitaji la Mwokozi. Kwa Kiebrania, neno dabarim (Kut. 34:28; Kum. 4:13; Kum. 10:4) lina maana pana kuliko “amri” pekee; linaweza pia kumaanisha “maneno” au “ahadi” (1 Fal. 8:56; Kum. 6:3). Hivyo, Amri Kumi ni ahadi za Mungu za kutuongoza na kutubariki tukizitii. Ellen G. White aliandika kwamba ni “ahadi kumi” za upendo wa Mungu kwa watu Wake. Paulo pia asema Kristo ndiye telos ya sheria (Rum. 10:4), si kwa kuiondoa, bali kama lengo lake kuu na utimilifu wake wa kweli. Sheria inabaki kuwa halali na yenye mamlaka (Rum. 3:31; 1 Kor. 7:19; Gal. 5:6), lakini kazi yake ni kutuongoza kwa Yesu, ambaye ndiye suluhisho la dhambi zetu na ukamilisho wa mapenzi ya Mungu ndani yetu.
#YesuNiUtimilifuWaSheria #SheriaNaNeema #AhadiZaMungu #AmriKumi #KristoLengoLaSheria #Biblia #MaishaKamili
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: