MABASI YA MWENDOKASI ZAIDI YA 900 YANATARAJIWA KUWASILI NCHINI, YATAHUDUMU MBAGALA, KIMARA
Автор: Millard Ayo
Загружено: 2025-08-04
Просмотров: 7856
Описание:
Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wanatarajiwa kushuhudia mabadiliko makubwa ya mfumo wa usafiri ifikapo mwezi Oktoba, 2025, baada ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kutangaza kuingiza zaidi ya mabasi zaidi ya 900 mapya katika mradi wa BRT.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa DART, Dk. Athumani Kihamia, ambapo amesema mabasi 755 yatahudumu kwenye njia ya Mbagala kwenda Mjini, na mabasi 177 katika njia ya Kimara kuelekea Mjini.
Aidha Dk, Athumani Kihamia Ameeleza kuwa Lengo ni kuhakikisha kwamba changamoto ya kungojea kwa muda mrefu vituoni pamoja na msongamano wa watu zinapungua kwa kiwango kikubwa na changamoto ya usafiri kwa wakazi wa Dar es Salaam itakuwa historia.
Kwa mujibu wa Dk. Kihamia, mabasi hayo yanatarajiwa kuanza kuingiza nchini mwezi huu Agosti, Septemba na mwisho ni Oktoba mwaka huu kukamilisha idadi ya zaidi 900 huki hatua hiyo inatarajiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa utegemezi wa magari madogo binafsi na hivyo kupunguza msongamano wa magari katikati ya jiji.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: