MRADI MKUBWA WA GESI TANGA KUCHOCHEA MATUMIZI YA NISHATI SAFI.
Автор: CLOUDS HABARI
Загружено: 2025-06-06
Просмотров: 110
Описание:
MRADI MKUBWA WA GESI TANGA KUCHOCHEA MATUMIZI YA NISHATI SAFI
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko, amesema kuwa matumizi ya nishati safi ya kupikia yameongezeka kwa kasi nchini, ikilinganishwa na miaka ya nyuma, kutokana na juhudi za serikali katika kusimamia utekelezaji wa sera na kuhamasisha matumizi ya nishati hiyo salama kwa afya na mazingira.
Dkt. Biteko ameyasema hayo wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la mradi mkubwa wa miundombinu ya gesi ya kimiminika (LPG) unaotekelezwa katika Kijiji cha Chongoleani, Jijini Tanga.
Mradi huo unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya kampuni ya ASAS na kampuni ya Petredec yenye makao makuu nchini Singapore, na unakadiriwa kugharimu takribani Dola za Marekani milioni 100.
Kwa upande wake, Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Selemani Jafo amesema serikali ina mpango wa kujenga viwanda 948 kote nchini, ambapo Mkoa wa Tanga ni miongoni mwa maeneo yatakayonufaika na utekelezaji huo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Batilda Burian amesema kuwa kupitia mradi huo mkubwa wa gesi, Mkoa wa Tanga unatarajia kupata ajira mpya kwa wananchi pamoja na kuongeza mapato ya mkoa kwa ujumla.
Mwakilishi kutoka ASAS Group, Ahmed Asas, amesema kuwa mradi huo ni sehemu ya mchango wa Tanzania katika kukuza usalama wa mazingira na kuunga mkono ajenda ya taifa ya matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: