WAISRAEL WAMKATAA NETANYAHU, WAIHOFIA HAMAS, WADAI UTAWAUA MATEKA WAO
Автор: Mwananchi Digital
Загружено: 2025-03-23
Просмотров: 50995
Описание:
“Kumechafuka.” Ndivyo unavyoweza kusema baada ya maelfu ya watu nchini Israel kuingia mitaani na kukusanyika katikati ya Jiji la Tel Aviv kupinga uamuzi wa Serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu wa kumfuta kazi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (Shin Bet), Ronen Bar
Pia maelfu ya raia hao wanaandamana kupinga uamuzi wa vikosi vya Jeshi la nchi hiyo (IDF) kurejea kwenye vita vya Gaza dhidi ya kundi la wapiganaji wa Hamas.
Netanyahu alisema wiki hii kwamba hana tena imani na Ronen Bar, ambaye amekuwa akiiongoza Shin Bet tangu 2021 huku akisema alikusudia kumfukuza kazi kuanzia Aprili 10, jambo lililosababisha maandamano ya siku tatu.
Jumamosi, kiongozi huyo wa Israel alisema nchi hiyo itaendelea kuwa ya kidemokrasia licha ya kufutwa kazi kwa mkuu wa usalama.
Katika Uwanja wa Habima mjini Tel Aviv, waandamanaji walipunga bendera za Israel za rangi ya buluu na nyeupe na kutaka kufikiwa kwa makubaliano yatakayowawezesha mateka waliobaki Gaza kuachiliwa.
“Adui hatari zaidi wa Israel ni Benjamin Netanyahu,” alisema Moshe Haaharony ( 63) alipokuwa akizungumza na shirika la habari la Reuters.
“Benjamin Netanyahu kwa miaka 20 hajali nchi, hajali raia wake.”
Netanyahu amekana madai kwamba uamuzi wake ni wa kisiasa, lakini wakosoaji wake wanamtuhumu kwa kudhoofisha taasisi zinazounda misingi ya demokrasia ya Israel kwa kutaka kumuondoa Bar.
Mahakama Kuu ya Israel ilitoa zuio Ijumaa, ikisitisha kwa muda kufutwa kazi kwa Bar. Hata hivyo, Bunge la Israel liliidhinisha uamuzi wa kufutwa kazi kwa Bar.
Netanyahu na Bar wamekuwa na mvutano kwa miezi kadhaa kutokana na uchunguzi wa rushwa unaomlenga waziri mkuu na lawama zinazotokana na kushindwa kuzuia mashambulizi yaliyoongozwa na Hamas mnamo Oktoba 7, 2023, kusini mwa Israel.
Katika barua yake, Bar alisema kufutwa kwake kazi kunalenga kusitisha harakati zake kutafuta ukweli kuhusu matukio yaliyopelekea Oktoba 7,2023 na kubaini ushiriki wa Netanyahu katika juhudi za kukwamisha kukoma kwa mapigano hayo anayodai yanagharimu maisha ya raia wa Israel.
Imeandikwa na Mgongo Kaitira kwa msaada wa Mashirika.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: