DMO ACHANGANYA MAELEZO MBELE YA WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA
Автор: Uyui FM Radio
Загружено: 2026-03-14
Просмотров: 315
Описание:
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba ameeleza kusikitishwa na vitendo vya Wananchi kuambiwa wakanunue dawa katika maduka ya mitaani ikiwa taarifa zinaonyesha dawa zinajitosheleza.
Mwigulu ameyasema hayo leo Machi 14, 2026 wakati akizungumza na Wananchi wa Kibaoni, katika Halmashauri ya Mpimbwe Mkoa wa Katavi baada ya kupokea malalamiko kuwa wanapoenda katika huduma za afya za Serikali wanaelekezwa kununua dawa katika maduka ya nje ya hospitali za Serikali.
Mwigulu amemuhoji Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mpimbwe kuhusu tuhuma hizo, ambapo amekiri kuwa baadhi ya Watumishi wamechukuliwa hatua kutokana na kadhia hiyo.
Aidha, Waziri Mkuu amemuelekeza kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa katavi kuhakikisha anafuatilia kwa undani suala hilo, ili kubaini iwapo kuna mianya ya rushwa na utoroshaji wa dawa za Serikali katika maduka hayo binafsi.
📻 Sikiliza Uyui FM Radio popote ulipo duniani, bofya kiungo (link) kwenye bio yetu.
#uyuifmradio #tunasambazaunyamwezi #Fanikisha #radioyetusautiyetu
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: