Ishara 7 Kwamba Unaongeza Hatua za Maendeleo, Matokeo na Mafanikio
Автор: LENZI | Michael Kamukulu
Загружено: 2025-02-17
Просмотров: 3405
Описание:
Maendeleo siyo ajali, ni matokeo ya juhudi, kujifunza, na uvumilivu. Katika video hii, tunajadili ishara 7 kwamba unapata HATUA za Maendeleo, Matokeo, na Mafanikio. Watu wengi hupitia mabadiliko haya wanapokuwa njiani kuelekea mafanikio yao. Kama unaziona dalili hizi kwenye maisha yako, basi fahamu kuwa uko kwenye njia sahihi! Ungana na Michael Kamukulu kupitia @lenzi.michaelkamukulu upate kujifunza zaidi kuhusu ishara jinsi ya kufanya ili uwe mtu wa tofauti, na upate fursa na nafasi ya kuinuka na kusimama imara ukiwa kiongozi na mwongoza njia wa maisha yako na kuwa na ushawishi kwa watu wengi. Utapata maarifa na ujuzi utakaokubadilisha na kuwa na tabia za watu wenye mafanikio na matokeo makubwa kifedha na kimaisha kwa ujumla. Ni wakati wako kung'ara na kuwa mtu wa thamani zaidi kwa wengine na kwa maisha yako. Utajiri na umasikini vyote viko kwenye nguvu ya tabia, mienendo na maamuzi yako ya kila siku.
Kwenye video hii utajifunza:
✅ Utapoteza marafiki wengi, utapata wapya wachache
Kadri unavyoendelea kubadilika na kukua, baadhi ya marafiki wa zamani hawatakuelewa tena. Utajikuta ukiwa karibu na watu wachache lakini wenye mawazo yanayolingana na safari yako ya maendeleo.
✅ Utapata ushindani kutoka kwa watu wa karibu
Mafanikio yako yanaweza kuwafanya watu wa karibu kuhisi wivu au kutokuamini mabadiliko yako. Hili ni jambo la kawaida – endelea mbele bila kuathirika na mitazamo hasi.
✅ Utabadilisha vipaumbele vya muda wako
Kama zamani ulikuwa unatumia muda mwingi kwa starehe au mambo yasiyo na tija, sasa utaanza kuwekeza muda wako kwenye vitu vyenye faida kubwa kwa maisha yako.
✅ Utapata fursa ulizokosa zamani
Ukiwa na mtazamo mpya na bidii, utaanza kuvutia fursa ambazo zilikuwa nje ya uwezo wako hapo awali. Maandalizi yako yatakutana na nafasi sahihi kwa wakati sahihi.
✅ Bidii itabadilika kuwa kipaumbele
Utaanza kutanguliza kazi na juhudi badala ya kutegemea bahati. Hii ni ishara muhimu ya ukuaji wa kweli.
✅ Utapendelea matokeo yako
Kadri unavyofanikisha malengo yako, utajikuta ukifurahia maendeleo yako kuliko maoni ya wengine. Furaha yako itategemea matokeo ya juhudi zako.
✅ Hautajali maneno ya watu
Watu watasema chochote, lakini wewe utakuwa na msimamo wako. Hutahisi hitaji la kuthibitisha thamani yako kwa mtu yeyote.
Usisahau ku-LIKE, KU-COMMENT na KU-SUBSCRIBE ili upate mafunzo zaidi!
———————————————
Wasiliana nasi kwa huduma zaidi ikiwemo:
1. Mafunzo na mwongozo maalum wa kufikia malengo (personal/individual coaching)
2. Mafunzo na mwongozo maalum kwa makundi na taasisi (group coaching)
3. Ushauri wa kitaalam kuhusu maendeleo binafsi (personal development)
Mawasiliano yetu:
Simu: +255 752 465 039
Baruapepe: [email protected]
* *
Pata Kozi Kuhusu jinsi ya kujiajiri na kuongeza kipato kwa kutumia MAUDHUI kwa bei nafuu ya TZS 15,000 tu kupitia hapa https://tr.ee/UTrb-ghbfk
#HatuaMojaMbeleKilaSiku #michaelkamukulu #lenzimindset #lenziacademy
* *
Chapters
00:00 Ishara 7 kwamba unapata HATUA za Maendeleo
00:42 1. Utapoteza marafiki
02:24 2. Utapata ushindani
03:27 3. Utabadilisha vipaumbele
04:04 4. Utapata fursa za zamani
04:52 5. Bidii itakuwa kipaumbele
05:26 6. Utapendelea matokeo yako
06:32 7. Hautajali maneno ya watu
07:33 Hitimisho.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: