ycliper

Популярное

Музыка Кино и Анимация Автомобили Животные Спорт Путешествия Игры Юмор

Интересные видео

2025 Сериалы Трейлеры Новости Как сделать Видеоуроки Diy своими руками

Топ запросов

смотреть а4 schoolboy runaway турецкий сериал смотреть мультфильмы эдисон
Скачать

Kimasomaso -Issa Matona

Автор: Zanzibar orchestra

Загружено: 2025-09-19

Просмотров: 18958

Описание: Aye masomaso mwanangu asimuone
Kimasomaso mwanangu asimuone
Kwa jicho la hasidi mwanangu asimuone
Ah na wambaya wetu eeh mwanetu asimuone
Masooo mwanangu asimuone

Hongera mwanangu eeh hongera
na mimi mamae tuhongere
Nasema yuwapi weeh
yuwapi mamae harusi aje hapa tuhangaike nae
nasema yuwapi jamani leo
yuwapi mama
Na mamae harusi namtaka aje hapa
Shangazi lake harusi nae namtaka aje hapa
Na dadaake harusi nae namtaka aje hapa
Na bibiake nae namtaka aje hapa
na somo yake harusi namtaka aje hapa
tuje tumfunze mwari asije kufedheheka
ukiitwa na mumeo mama wajibu kumuitika
ukiitwa ewe bibi uitike bwana labeka
umridhie mumeo mama kwa kila analotaka

ijapokuwa na mwao sitaki mnitukane
nnawaita wazazi waje hapa tuonane
wanipe mkaja wangu upatao mia nane
umuweke utangani mwari amsemeza aseme
uinue uso nyuma mama wahisani uwaone
uangaze kila pembe na wabaya uwaone
anapokuwa mumeo hujambo muulizane
uufungue mkoba mama kilo ndani ukione
utahadhari na shoga wasije wakunyang’anye
salkheri njiani wengine si wanaume
leo umepata wako mahawara na wakome

hodi hodi nnakuja kuja na langu shauri
mlombali msogee wala msitaakhari
makungwi mkusanyike imeingia hatari
vifunikavyo vyaliwa vinaachwa vilowazi
mwari amevunja ungo mutahadhari walezi

somo yake biharusi hebu nitafutieni
na kungwi lake harusi wote waje hapa uwanjani
tuje tumfunze mwari malezi ya kizamani
unapopelekwa kwako mama unapofika nyumbani
ukacheke na mumeo mama umpumbaze chumbani
wakaja na ndugu zako wakaribishe chumbani
wakaja mawifi zako mama uinuke kitandani
wanapokuja wakwezo uwaweke ukumbini
wakaja shemegi zako uwaweke barazani
wakaja mashoga zako sema nao dirishani
wakikuaga kwaheri uwambie karibuni
ufunge mlango wako urejee kitandani
huku ukichekacheka na macho yawe laini

nasema na dada zangu nyie mnaokaa mjini
nyie mnao waume leo sikizeni kwa makini
karandinga limelia vibaibui begani
muwazuwie waume wasirande majiani
muwafunge kwa vitanzi muwafiche maziwani
akija akikutoka mume humuoni asilani
atapikiwa mkate na vichuzi bakulini
atafukizwa na udi na asumini kitandani
atakupita na honda yule sie bwana khalfani
utolewe kwate lako ulie na mito kitandani

ndugu zangu maharusi sikizeni nnasema
tumengia mitamboni watu wote wanaona
wazazi wa mke na mume wote wamekusanyana
huu ni wangu wasia msiseme natukana
mashoga wa siku hizi ujue hawana maana
mkikutana njiani eti hujambo huulizana
utamfanya mpenzi siri zenu kupeana
umkaribishe njiani furaha na taadhima
utampikia dhifa nyingi nyingi zilonona
umuoneshe wazazi huyu baba huyu mama
ukimuonesha shemegi atamwinukia wima
atafanya kila mbinu apate kumuandama
fadhila na ihisani hatozikumbuka tena
akuache unalia njiani unalalama
utatamani akhera nawe ungali mzima

kama atakwita bibi nimekuzalia nani
miezi miwili mitatu mama mibegi yako kichwani
huu ni wangu wasia Issa nnasema uwanjani
sikizeni kwa makini nyie wari mlovipembni

ukaisikia hodi mama ushungi uwe kichwani
huenda akawa mumeo mama usimkere moyoni
kama ndie bwana pita kwa sauti ya huzuni

Не удается загрузить Youtube-плеер. Проверьте блокировку Youtube в вашей сети.
Повторяем попытку...
Kimasomaso -Issa Matona

Поделиться в:

Доступные форматы для скачивания:

Скачать видео

  • Информация по загрузке:

Скачать аудио

Похожие видео

Swahili: Bure

Swahili: Bure

BI RUKIA AKIIMBA

BI RUKIA AKIIMBA "HUJAFA HUJAUMBIKA" KWA HISIA KUBWA, MANARA AMWAGA PESA, LAYLATUL HELWA

Эпичный вестерн | Дикий Мститель крушит врагов государства | Боевик | Вестерн | Фильм

Эпичный вестерн | Дикий Мститель крушит врагов государства | Боевик | Вестерн | Фильм

SIBAGUI SICHAGUI  :   Zuhura Shaban.  #taarab

SIBAGUI SICHAGUI : Zuhura Shaban. #taarab

Mke Kumpa Talaka

Mke Kumpa Talaka

subira(huvuta heri) -  Khadija baramia #taarab #oldisgold #zanzibarmusic #swahilimusic

subira(huvuta heri) - Khadija baramia #taarab #oldisgold #zanzibarmusic #swahilimusic

DEDES WA ZNZ AIPAMBA ANAYO ALAMA, BALOZI ATOA MILION 1 IRUDIWE, TAMASHA LA USIKU WA FARAJA

DEDES WA ZNZ AIPAMBA ANAYO ALAMA, BALOZI ATOA MILION 1 IRUDIWE, TAMASHA LA USIKU WA FARAJA

Taarab Zanzibar:Aso kasoro hakuna -Fatma issa ||taarab zilipendwa ||taarabu za zamani

Taarab Zanzibar:Aso kasoro hakuna -Fatma issa ||taarab zilipendwa ||taarabu za zamani

DUMBAKI  JKU DOLE

DUMBAKI JKU DOLE

Leo tena - Abdallah issa| swahili taarab|taarab asilia zanzibarl|zanzibar songs |Abdallah issa songs

Leo tena - Abdallah issa| swahili taarab|taarab asilia zanzibarl|zanzibar songs |Abdallah issa songs

Sibasi tu -Abdalla Issa@Al ghafri

Sibasi tu -Abdalla Issa@Al ghafri

Nikumbatiye/Seleleya by Rukia Ramadhan (new version)

Nikumbatiye/Seleleya by Rukia Ramadhan (new version)

mapezi yako matamu ya salamu - Khadija Baramia all somgs #taarab #oldisgoldzanzibar#taarab

mapezi yako matamu ya salamu - Khadija Baramia all somgs #taarab #oldisgoldzanzibar#taarab

SHAMBA LIMESHAKUSHINDA

SHAMBA LIMESHAKUSHINDA

Usihofu kizare

Usihofu kizare

Bora Adui Shetani Kama adui Kiumbe Fatma Issa

Bora Adui Shetani Kama adui Kiumbe Fatma Issa

MAKAME FAKI | NIMELETWA DUNIANI KWA AJILI YAKO - NDO NYIMBO NZURI YAO TANZANIA

MAKAME FAKI | NIMELETWA DUNIANI KWA AJILI YAKO - NDO NYIMBO NZURI YAO TANZANIA

MSUMENO / ISSA MATONA /JKT TARAAB

MSUMENO / ISSA MATONA /JKT TARAAB

Poa Moto mke wangu - Abdalla Issa

Poa Moto mke wangu - Abdalla Issa

Jitoe Kimasomaso - mwanahawa ally with East African Melody (live)

Jitoe Kimasomaso - mwanahawa ally with East African Melody (live)

© 2025 ycliper. Все права защищены.



  • Контакты
  • О нас
  • Политика конфиденциальности



Контакты для правообладателей: [email protected]