KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 09/02/2026
Автор: KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH
Загружено: 2026-02-10
Просмотров: 3249
Описание:
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 09/02/2026
UJUMBE WA LEO:
MAMBO YATAKAYOKUWEZESHA KUTOKA NYUMBA YA UTUMWA MPAKA UTIMILIFU WA AHADI
Kutoka 20 : 1 - 2
Kutoka 3 : 7 - 9
Mwanzo 16 : 13 - 14
1. Kuelewa Safari ya Ukombozi na namna udhihirisho wa mkono wa MUNGU kuingilia kati hali za watu wake waliopo kwenye nyumba ya utumwa.
2. Nafasi ya Agano la urithi na mauti kutoka kwenye madhara yake ili kunufaika kwa kutoka katika nyumba ya Utumwa.
3. Kujua dalili ya vita inayolenga kipawa chako, ili kubakia utumwani kama lengo la Adui kisitumike kukutoa Utumwani.
Kutoka 20 : 1 - 2
1 Mungu akanena maneno haya yote akasema,
2 Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.
Kutoka 3 : 7 - 9
7 Bwana akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao;
8 nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi.
9 Basi, tazama, kilio cha wana wa Israeli kimenifikilia; tena nimeyaona hayo mateso ambayo Wamisri wanawatesa.
Mwanzo 16 : 13 - 14
13 Akaliita jina la Bwana aliyesema naye, Wewe U Mungu uonaye, kwani alisema, Hata hapa nimemwona yeye anionaye?
14 Kwa hiyo kisima kile kiliitwa Beer-lahai-roi.c Tazama, kiko kati ya Kadeshi na Beredi.
SAFARI YA UKOMBOZI INA HATUA TATU.
1. Mungu anaona utumwa.
2. Mungu anaingilia kwa mkono wake
3. Mungu anatimiza ahadi yake kwa wakati wake.
1. Mungu anatambua hali ya mateso na vifungo vya watu wake.
Kutoka 3 : 7
“Bwana akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri…”
Hakuna mateso yaliyo fichika mbele za Mungu.
Hakuna kifungo kinachomshinda Mungu kukitambua.
Utumwa wako haupuuzwi wala kusahaulika.
Mungu anaona maumivu, dhuluma, machozi, na ukandamizaji.
Ni jina la Mungu katika Biblia lenye maana nzito sana kiroho.
El Roi maana yake ni;
“Mungu anayeona” au “Mungu anayeniona.”
Ni Mungu ambaye haoni kwa jumla tu, bali anamuona mtu binafsi, hali yake, maumivu yake, na kilio chake.
1. OMBA TOBA ILI KUJINASUA KATIKA UHALALI WA UOVU AU DHAMBI INAYOKUSHIKILIA UTUMWANI.
1 Yohana 1 : 8 - 9
8 Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.
9 Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.
2. OMBA MUNGU AJIDHIRISHE KAMA (EL-ROI) MUNGU AONAYE MAHALI AU HALI YA MATESO AU VIFUNGO VYAKO KAMA NYUMBA YA UTUMWA.
Kutoka 3 : 7
7 Bwana akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao;
Mwanzo 16 : 13
13 Akaliita jina la Bwana aliyesema naye, Wewe U Mungu uonaye, kwani alisema, Hata hapa nimemwona yeye anionaye?
Mhubiri : Mwl.Renald Mlawi.
Kwa maombi na ushauri :
Mch. Kiongozi: Dr. Eliona Kimaro
Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053
Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga
Simu: +255 713 553 443
YouTube: Kijitonyama Lutheran church
Barua Pepe : [email protected]
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: