SERIKALI YATOA BILIONI 323 UWEZESHAJI WA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU
Автор: KIZURI DGITAL
Загружено: 2026-03-09
Просмотров: 20
Описание:
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, amesema kuwa Serikali kupitia mamlaka za Serikali za Mitaa imeendelea kutoa mikopo isiyo na riba kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa lengo la kuwawezesha kiuchumi.
Amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitano, 2021/2022 hadi Desemba 2025, jumla ya shilingi bilioni 323 zimetolewa kwa vikundi 35,526 vya walengwa hao nchini.
Dkt. Gwajima alifafanua kuwa kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 159.8 zimetolewa kwa vikundi 19,959 vya wanawake, huku Mkoa wa Geita pekee ukipokea zaidi ya shilingi bilioni 4.8 kwa ajili ya kuwawezesha wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Aidha, Dkt. Gwajima amesisitiza kuwa uwezeshaji wa wanawake kiuchumi sio kauli ya kisiasa, bali ni ajenda ya kitaifa inayotekelezwa kwa vitendo, kwa kutumia rasilimali za fedha na kuleta matokeo yanayoonekana katika jamii.
Dkt. Gwajima amesema hayo wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika tarehe 8 Machi 2026 mkoani Geita
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: