Muwezeshe Atembee
Автор: GSM GROUP OF COMPANIES
Загружено: 2026-03-02
Просмотров: 16
Описание:
GSM Foundation inaendelea na kampeni yake ya "Muwezeshe Atembee" kwa kushirikiana na CCBRT, klabu ya mpira ya YANGA, kampeni inayolenga kusaidia matibabu ya watoto wenye changamoto za Mguu Kifundo (clubfoot)
Mnamo mwaka jana, Machi 2025, GSM Foundation iliongoza harambee iliyofanyika jijini Daresalaam na na kufanikiwa kupata michango kutoka Taasisi za serikali,Asasi za kiraia, makampuni, na watu binafsi, na mpaka sasa watoto takribani 300 wameweza kupatiwa matibabu hayo katika hospitali ya CCBRT.
Leo, Mkuu wa GSM Foundation ,Bi Faith Gugu akiambatana na timu ya watendaji wa GSM Group na CCBRT, wamemtembelea mmoja wa wanufaika wa programu hiyo anayeishi Mkuranga, Pwani.
GSM Foundation pia ilipeleka zawadi za bidhaa za mahitaji ya nyumbani zinazozalishwa na kampuni za @gsmbeverage na @gsmgroupofcompanies ili kuifariji familia hiyo.
GSM Foundation inawashukuru wadau wote waliochangia na kuwakaribisha wadau wengine kuendela kujitokeza kuunga mkono kampeni hii.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: